Eva: Amenambia nikuamini wewe ni baba mzuri, unanipenda kama ambavyo mama ananipenda.
Damian: Usiogope mwanangu baba yako hajakudanganya, unachotakiwa ni kumsikiliza baba yako alichokuambia.
SIKU ILIYOFUATA.
Eva anaamka asubuhi mapema, anakula chakula cha asubuhi baada ya hapo anafanya kazi ndogo ndogo za nyumbani, baadae mida ya saa 7: 00 mchana anakula chakula cha mchana na kusoma vitabu baadae mida ya jioni mama yake anarudi kutoka kazini. Gari nzuri aina ya Rolls Royce inaingia katika jumba lile la kifahari anashuka mama yake Eva pamoja na baba yake wa kambo.Eva anawaona anatoka ndani anaenda kuwapokea.
Joyce: Woooow!! Mwanangu kipenzi Evaa, umeshindaje binti yangu..?
Eva: Nimeshinda salama, shikamo mama.
Joyce: Marahaba mwanangu, nilikukumbuka sana.
Eva: Nimekukumbuka pia mama... Leo nime-enjoy kushinda hapa nyumbani, ni pazuri.
Joyce: Wooow!! vizuri mtoto wangu mzuri, nafurahi kusikia mwanangu umepapenda nyumbani.
Eva: Oohh!! lakini nimeshindwa kufanya kitu kimoja...
Joyce: Kipi hicho mwanangu ?
Eva: Leo sijaongea na baba.
Joyce: Kwanini sasa..!?
Eva: Naona simu yangu kama inashida kwenye mtandao toka asubuhi.
Damian akamjibu...
Damian: Usijari Eva nitahakikisha unaongea na baba yako.
Eva: Wow!! nitafurahi sana baba.
Damian: Usijari mwanangu njoo uongee na baba yako.
Eva akaondoka pamoja na baba yake wa kambo wakaenda kukaa sehemu ya kupumzikia ambayo imejengwa vizuri kwa mfano wa nyumba ya msonge, pembeni kidogo ya kijumba hicho cha msonge kuna swiming pool kubwa lenye umbo duara. Sehemu hiyo inaupepo mzuri kutokana na miti mizuri ya aina mbalimbali iliyozunguka eneo hilo. Damian akatoa simu yake, akampigia Mr Moses kwa njia ya video (video call). Wakati huo Mr Moses alikuwa kazini simu yake ikaita.
Mr Moses: Ooh!! naona Mr Damian kanitafuta…!
Akapokea
Eva: hallooo baba..!!
Mr Moses: halloo Eva!, hujambo mwanangu.
Eva: Sijambo baba, nimekukumbuka kweli baba yangu kipenzi, sijui nitakuja lini kukuona.
Mr Moses: Nimekukumbuka pia Eva wangu, likizo ikisha tu nitakuja kukuchukua... Ila hujawasumbua kweli baba na mama?
Eva: Hapana sijawasumbua hata, nimefanya kila kitu ambacho nilikua nafanya nikiwa huko.. Ninafuraha sana, mama ananipenda na baba pia ananipenda sana.
Mr Moses: Woow! Nilikuambia utanisahau tu (utani)
Eva: Siwezi kukusahau baba yangu, iyo siku haipo.
Mr Moses: Najua hilo mtoto wangu, nilikuambia baba pamoja na mama yako wanakupenda.. Sasa unajionea mwenyewe.
Eva: Ndio baba sahivi naelewa.
Muda huo simu ya ofisini ilikua inaita, ikabidi Mr Moses amuage mtoto wake ili apokee ile simu nyingine.
Mr Moses: Aya!! Sawa Eva nitakutafuta kesho saivi napigiwa simu ofisini. Sawa byee!!
Eva: Byee!! Nakupenda sana baba.
Mr Moses: Nakupenda sana pia binti yangu.
Mr Moses akakata simu ya Eva kisha akapokea ile simu ya ofisini iliyokuwa inaita.
Mr Moses: hallo.
Mfanyakazi (mapokezi): Boss tayari waandishi wamefika eneo husika, wanakusbiri wewe tu.
Mr Moses: Sawa nakuja sasa hivi.
Upande wa Eva akiwa na baba yake wa kambo Mr Damian.
Damian: Umefurahi sana kuongea na baba yako?
Eva: Ndio nimefurahi sana, nampenda sana baba yangu.
Damian: Mmhh!! kati ya baba na mama yako unampenda nani zaidi?
Eva: Nampenda zaidi baba.
Damian: Mmh!! kwanini baba na sio mama?
Eva: Kwasababu yeye amekaa na mimi siku zote, ila mama yeye aliniacha akaja huku. (kwa kujiamini)
Damian: Ooohh!!Mungu msamehe binti huyu, anahukumu bila kujua chochote.(kwa sauti ya chini)
Eva: Kwanini Mungu anisamehe?
Damian: Nasikitika hujui nini sababu ya mama yako kuja huku na kwanini alikuacha wewe huko pamoja na baba yako.
Eva: Kwanini mama aliniacha na kuja huku?
Damian: Nikikuambia utaniamini?
Eva: Ndio nitakuamini ikiwa ni kweli… Ila kwanini unaogopa siwezi kukuamini?
Damian: Kwasababu unamuamini sana baba yako.
Eva: Ndio baba yangu namuamini sana.
Damian: Hilo ndio kosa ulilofanya na ndio sehemu ambayo baba yako amefanikiwa.
Eva: Kivipi..!?
Damian: Baba yako amefanikiwa kukufunga akili yako umuamini yeye tu. Hii ndio sababu huwezi kuamini wengine. Unajiuliza kwanini sasa amefanya hivyo…? Amefanya hivyo ili usiujue ukweli mbaya ambao upo nyuma ya kutengana na mke wake, mama yako.
Eva: Sawa niambie sababu ni nini.
Damian: Sawa nitakuambia ila nasikitika baba yako amekupumbaza sana… Ukweli ni kwamba Baba yako ni mtu mbaya sana,baba yako ni mtu mkorofi sana, baba yako ndio aliefanya ukae mbali na mama yako. Baba yako huyo huyo unaempenda alikua anampiga sana mama yako, anamnyanyasa, anamtukana sana. Baba yako anakuambia hajawai kuwa na mwanamke mwingine anakudanganya.
Eva: Muongo!! umewezaje kujua hayo yote?
Damian: Mimi nilikutana na mama yako akanieleza yote hayo. Kwakua sikupendezwa na alichokifanya baba yako na nilikua bado sijaoa nikaamua kuishi na mama yako na kumfanya awe na furaha tena kama ulivyomkuta sahivi. Pia mama yako aliniambia ana-mtoto ambae ni wewe kwahiyo nikafanya jitihada niwezavyo ili nikulete tukae wote. Lakini yote hayo huyajui.
Eva: We muongo!! Nitakuamini vipi? Baba yangu hayupo hivyo, namjua.
Damian: Kama huniamini basi, ila kesho muulize mama yako akuthibitishie labda akisema yeye utamuamini. Lakini kumbuka nimekuambia hayo sio kwajili unipende na kuniamini mimi ila nimekuambia ili upendo uliompa baba yako umpe mama yako, kwasababu ndie anaestahiri upendo huo.
Eva: Sawa nenda, niache kwanza. (kwa hasira)
Damian: Sawa Eva najua nimekumiza lakini ndio ukweli. Aya badae mwanangu.
Eva akabaki na mawazo mengi akiwa pekee yake pale sehemu ya kupumzikia. Akijiuliza maswali na kujibu mwenyewe. Akakumbuka baba yake alimwambie kuwa yeye ndie alimkosea mama yake.
Eva: Baba kweli wewe ndio ulimfanyia hivi mama, ulikukosea nini mama, baba sema sio ya kweli haya.
Upande wa Mr Moses akiwa ofisini kwake na waandishi wa habari.
Mr Moses : Kwa mwaka huu tumejipanga kuboresha huduma zetu kuwa nzuri zaidi tofauti na miaka iliyopita, kama mnavyojua kampuni yetu iliyumba kidogo miaka kadhaa iliyopita baada ya kufarakana kati yangu mimi na aliyekuwa mke wangu na mshirika wangu wa biashara Madam Joyce, lakini sasa na ahidi tumerudi kwenye mstari kama awali.
Wakati akiendelea na mazungumzo mwandishi mmoja alitumiwa sms:
Sms: Akiruhusu swali la mwisho, mulize lile swali.
Mr Moses: Ok!! niruhusu swali la mwisho... Eeeehh!! ok pale nyuma we uliza?
Mwandishi: Mmh!! Asante Mr Moses, Swali langu ni kuhusu aliekuwa mke wako pmaoja na mshirika wako wa biashara Madam Joyce, kwasababu na yeye umemgusia kwenye mazungumzo yako, watu wanataka kujua kuhusu madai ya kwamba ulikua ukimtolea lugha chafu,kumpiga na kumfanyia matendo mengine ya unyanyasaji kwa mwanamke, vipi unalizungumziaje hili!?
Mr Moses: Ooohhpp!! Ni kweli unayoyasema, mi' pia nayasikia, lakini hayana ukweli wowote zaidi ni ushindani wa kibiashara na makampuni mengine ikiwemo kampuni yake Madam Joyce ambayo pia ni mshindani wetu, so… jambo hili halina ukweli. Mimi na yeye tuliachana vizuri kwa makubaliano ya wote wawili na ukweli yeye ndio aliomba taraka, nikajaribu kutatua ikashindikana ndio maana leo hatupo pamoja. Huo ndio ukweli sio hayo mengine unayoyasikia. Asanteni.
Baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari Mr Moses alitambulisha toleo la nguo mpya kutoka kwenye kampuni yao. Nguo waliyoipa jina Daughter (binti) nguo kwajiri ya watoto wa kike.
Mr Moses: Sasa nawakaribisha kutazama toleo letu jipya la nguo,Nguo imetengenezwa kwa kuzingatia asiri ya kiafrika zaidi na nguo hii inaitwa Daughter mbunifu wa vazi hili ni Eva binti yangu pamoja na mimi mwenyewe kwenye baadhi ya vitu. Nguo hii tumetoa matoleo kwa kuzingatia kila lika. Karibuni sana.
Watu: hongera sana style nzuri ya nguo, inavutia sana./ Woow nimependa sana hii/ Itapatikana wapi/ Inauzwa shi-ngapi n.k.
*** ITAENDELEA ***
Soma hapo chini kwenye description kujua yaliyomo kwenye episode ijayo.

Comments (6)
See all