SIKU ILIYOFUATA
Ni siku ya mapumziko weekend Mama Eva (Joyce) hajenda kazini na leo yupo jikoni akipika chakula kwajili ya mlo wa mchana, Eva akaenda jikoni alipo mama yake.
Joyce: Eva mwanangu mbona unaonekana leo hauna furaha, Kuna nini mwanangu kipenzi. Sijazoe kukuona ukiwa hivyo!?
Eva: Hapana mama, hamna kitu hata. (Akatabasamu)
Joyce: Nambie mwanangu wala usiogope, mama yako nimeona haupo sawa.
Eva: Sawa mama.
Joyce: Aya nambie mwanangu kipenzi.
Eva: Je ni kweli aliyoniambia baba wa kambo?
Joyce: Oooh!! kumbe shida ni hilo tu mwanangu.
Eva: Ndio mama, nataka kujua.
Joyce: Ndio yote aliyokuambia baba yako wa kambo ni ya kweli, unatakiwa umuamini baba yako wa kambo kama unavyo muamini baba yako Mr Moses na hata baba alikuambia huyu ni baba yako pia, sawa Eva.
Eva: Sawa, nakupenda sana mama yangu, sijui kwanini sikukaa pamoja na wewe muda wote huo.
Joyce: Mi pia nilitamani kuwa na wewe mwanangu muda wote.
Eva: Sawa mama ngoja mi niende nikaangalie tv.
Joyce: Sawa mwanangu mi namalizia kuweka mambo sawa hapa ili ule ushibe.
Baada ya Eva kutoka Damian akaingia jikoni alipo Joyce, akaingia kwa kunyata akamkumbatia kwa nyuma huku mikono yake yote miwili akipitisha kiunoni.
Damian: Naona unaongea na binti yako.
Joyce: Ndio!! Lakini nashangaa leo hana furaha kabisa.
Damian: kwani anasemaje?
Joyce: Anauliza maswali kuhusu baba yake, wewe.
Damian: Na wewe umemjibu nini?
Joyce: Nimemjibu kama inavyotakiwa.
Damian: Sawa vizuri kumwambia mtoto ukweli.
Walipokuwa wakizungumza wakasikia sauti ya Eva akiwaita.
Eva: Mama mama!! Njoo umuone baba kwenye tv.
Mama yake pamoja na baba yake wa kambo wakatoka jikoni wakaenda sebureni kuangalia, yalikuwa ni mahojiano yale ya Mr Moses wakati anafanya uzinduzi wa nguo yao mpya kutoka katika kampuni yake, wakasikiliza kwa makini mpaka ilipofikia wakati anaulizwa swali kuhusu kumnyanyasa mkewe... Ukimya ulitawala kidogo kudhihirisha wote wanasikiliza kwa makini. Eva pia anataka kumsikia baba yake anajibu nini. Akasikiliza...
( Mr Moses: ooohh!! Ni kweli unayoyasema…) tv ikazima ghafla!!.
Joyce: Eva kwanini umezima tv!? (kwa hasira)
Eva: Hapana mama!! Yani hata sielewi.
Eva akanyanyuka akaenda chumbani kwake. Mama Eva (Joyce) akachukua rimoti akawasha tv akaendelea kuangalia mahojiano yale. Lakini chumbani alipo Eva pamewaka moto, Eva anahasira, kachukua picha ya baba yake akaitupa chini…
Eva: Baba!! Wewe ni mbaya hivi!? wewe ni mbaya, nakuchukia baba, nakuchukia sana aaahhh!! Kwanini ulimtesa mama yangu. Kwaniniiii…!! (Akiwa anainyoshea kidole ile picha)
BAADA YA WIKI MOJA.
Mr Moses amemkumbuka sana binti yake. Umepita muda mrefu hawajawasiliana na Eva.
Mr Mose: Nimekuwa bize sana, ni wiki moja sasa sijawasiliana na binti yangu, ngoja nimpigie.
Akapiga simu ya Eva lakini ikaita haikupokelewa ikabidi ampigie mama yake, akampigia Madam Joyce akapokea…
Mr Moses: hallo!!?
Joyce: Eeeh hallo!!
Mr Moses: Samahani kwa usumbufu, nashida na Eva nampigia simu yangu lakini hapokei.
Joyce: Ok! ngoja nimuite uongee nae.
: Eva, Evaa njoo uongee na baba.
Eva: Baba mbona nimetoka kuongeanae sahivi!
Joyce: Baba yako Mr Moses.
Eva: Hapana sitaki… sitaki kuongeanae.
Joyce: heeehh!! hutaki?
Eva: Ndio!!
Joyce: Amekataa kuongea na wewe eti.
Mr Moses: Shida nini!? Kuna tatizo gani kwani?
Joyce: Sifahamu, ila toka wiki iliyoisha hana raha kabisa. Lakini nafikiri atakaa sawa tu.
Mr Moses: Labda itakuwa amekasilika maana sijamtafuta wiki nzima.
Joyce: Inawezekana.
Mr Moses: Sawa Joyce, mwambie baba nampenda.
Joyce: Wala usijari nitamuambia.
Mr Moses: Joyce nakukumbuka sana. (Kwa sauti ya chini)
Joyce: Naku-miss sana pia Moses, lakini hatuwezi kuwa pamoja tena.(Kwa sauti ya chini)
Mr Moses: Yeah kweli!! Ok vipi leo hujaend kazini? (Akapotezea)
Joyce: Ndio leo sijaenda, sahivi kila kitu anasimamia Damian na muda sio mrefu amenda kazini.
Mr Moses: Vizuri, naona mnashirikiana. Ok poa utamsalimia Eva.
Joyce: Aya sawa byee.
Mr Moses: byee.
Kazini katika kampuni ya madam Joyce inayoitwa JOY (Furaha). Mr Damian akiwa ofisini anaongea na simu.
Damian: Wewe nivumilie tu… Sahivi imebaki kidogo tu… Aaaah! Siwezi kusahau nakumbuka makubaliano tuliyokubaliana na sahivi nataka nichukue na ile nyingine.
Simu: Sawa mi nakutegemea. (sauti ya mwanamke)
Damian: Wewe usijari mi nitalikamilisha… byee!!
Baada ya kumaliza kuongea na mtu huyo kwenye simu yake Mr Damian akachukua simu ya ofisini kisha akapiga.
Damian: hallo!!, umefatilia vizuri toleo lao jipya?
Simu(mfanyakazi): Ndio boss nimkamilisha.
Damian: Ok! hakikisha tunatengeneza toleo zuri zaidi kuliko hilo la Mr Moses nataka liwe bora kuliko toleo lao.
*** ITAENDELEA ***
Comments (2)
See all