Vyuo vimefunguliwa baada ya likizo kumalizika. Eva akiwa pamoja na wanachuo wenzake, ulikuwa ni muda wa kutoka kwenda nyumbani kwa mbele kidogo alimuona baba yake Mr Moses. Lakini Eva hakumjali akaanza kwenda kwenye usafiri uliomuijia.
Mr Moses: Eva, Evaa nimekukosea nini mwanangu, Eva... Samahani tunaweza kutumia gari yangu maana kuna mambo nataka tuzungumze. (kwa upole)
Eva akamuonea huruma baba yake, akamsikiliza.
Eva: Dereva!!
Dereva: Naam.
Eva: Wewe nenda nitatumia usafiri mwingine leo.
Dereva: Sawa madam Eva.
Mr Moses: Asante! mwanangu kwa kunisikiliza.
Baba yake akamfunguli mlango wa gari mwanae akaingia kisha na yeye akapanda.
Mr. Moses: Eva hujambo?
Eva: Sijambo shikamo baba.
Mr Moses: Marahaba mwanangu, Eve mbona siku hizi sikuelewi!! uliniahidi nini baada ya likizo, kwamba utarudi nyumbani lakini sasa ni mwezi mmoja hautuki kuongea na mimi kwanini?
Eva: Hapana baba.
Mr Moses: Ila kunanini? Nambie mwanangu usiogope, nambie... Nambie ukweli.
Eva: Baba wewe ndio ulimkosea mama?
Mr Moses: Mmhh aaah!!
Eva: Si ndio baba, wewe ndio ulimkosea mama, uliniambia ndio ni wewe, nambie baba!? (kwa hasira)
Mr Moses: Ndio ni mimi.
Eva: Ni kwanini umnyanyase sasa?
Mr Moses: Mwanangu usikilize maneno ya kwenye mitandao,tv na maneno ya watu mama yako niliachanae bila ugomvi. Tulikubliana kwa amani. Usisikilize wananichafua tu.
Eva: Hapana we muongo, ulimtesa ulimpiga, ndio sababu hakukaa na mimi, we baba ni mbaya sikupendi, nakuchukia nakuchukia. (akiwa anali)
Mr Moses: Eva!!
Eva: Na wala sijasikia kwa watu,wala sijatoa mtandaoni, nimeambiwa na mama... Nimeambiwa na mama yangu.
Mr Moses akakanyaga breki kwa ghafla.
Mr Moses: Mam..mam…mama ndio amekuambia hivyo!!
Eva: Ndio mama, mama yangu anasema ukweli.
: Baba yangu na mama yangu ni wale niliwacha nyumbani. Na sio wewe tena.
Mr Moses: Eeee e e e Eva!!
Eva akashuka kwenye gari akaondoka, huku baba yake akibaki hana cha kusema akiwa kwenye siti ya dereva ameshika usukani.
Mr Moses : (Akawaza) Eva niliahidi hakuna kitakacho nitenganisha na wewe mwanangu,nilikuambia wewe ndio kila kitu kwangu, sasa umenichukia na wewe, umenichukia baba yako kwa tuhuma zisizo za kweli, nitafanya chochote niwezacho nikurudishe kwangu… Atawajibika kila alie kutoa kwangu, mpendwa wangu Eva. Nakupenda. (akiwa na hasira)
Mr Moses akachukua simu yake. Inaonekana kuna mtu anataka kuwasiliana nae, akamtumia sms.
Mr Moses: Tunaweza kuonana?
sms: Sawa, wapi?
*** ITAENDELEA ***
Comments (3)
See all