...
Ni katika chumba cha bafu, Mr Moses anaweka risasi kwenye bunduki ndogo aina ya bastora, inaonekana ndio wakati sahihi anaenda kuifanya kazi hiyo, muda huu. Akasogea kwenye kioo huku akiongea mwenyewe kwenye kioo hicho akiwa na hasira sana.
Mr Moses: Sasa nitakuwa wanavyotaka niwe.
Wakati akiongea mwenyewe kwenye kioo sms ikaingia kwenye simu yake.
Sms: Mi’ nimeshafika.
Mr Moses: Sawa nakuja sahivi.
Tunakuja upande mwingine katika hoteli moja kubwa ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano, Kuna gari moja ya kifahari inaingia kwenye hoteli hii kisha anashuka Madam Joyce akiwa amevaa gauni zuri lenye rangi nyekundu akitembea katikati ya walinzi (bodyguard) wawili. Baada ya kuingia hotelini anaenda kukaa katika meza kubwa ya VVIP iliyokuwa mafichoni kidogo. Inaonekana kuna mtu anakutana nae katika hoteli hii.
Baada ya dakika mbili anaingia Mr Moses katika hoteli hiyo hiyo, kisha ananza kutembea kuelekea kwenye meza aliyokaa Madam Joyce lakini kabla hajafika katika ile meza anazauiliwa na wale walinzi wawili.
Bodyguard-1: Samahani mheshimiwa hauruhusiwi kuingia hapa.
Joyce: Muache aingie, ndie niliekuja kwajili yake. karibu baba Eva.
Mr Moses: Asante!! Naona umechagua meza nzuri.
Joyce: Hii yote ni kwaajili yako.
Mr Moses: Ok sawa, vipi Eva hajambo?
Joyce: Eva hajambo, namshukuru Mungu.
Mr Moses: Ok!! tusipoteze muda nimekuja hapa kunajambo nataka kujua, ulimwambia nini Eva kuhusu kutengana mimi na wewe?
Joyce: Moses..!! nataka tupige stori hata kidogo na wewe siunajua ni muda mrefu hatujakaa meza moja kama tulivyokaa hivi leo.
Mr Moses: Samahani Joyce sipo hapa kwajiri ya hilo.
Joyce: Ok! Mi sijamwambia chochote Eva.
Mr Moses: Kwanini Eva analalamika nilikua namnyanyasa mama yake mpaka kupelekea mama yake kuondoka.(kwa ukali)
Joyce: Yeah!! Ni kweli..
Mr Moses: Huo ni upumbavu!! (akapiga meza)
Walinzi wakasogea lakini madam Joyce akawazuia.
Joyce: Tafadhari msimguse, tena samahani sana naomba mtupishe tunamaongezi ambayo hamtakiwi kusikia. Samahani sana.
Bodyguard: Sawa boss.
Walinzi wakaondoka wakaenda kukaa mbali wasipoweza kusikia kinacho zungumzwa.
Mr Moses: Joyce ukweli unaujua kwanini unamdanganya mtoto!!, unajua kabisa Eva ndio kila kitu kwangu lakini na yeye umeamua kumchukua tena kwa kumjaza chuki dhidi yangu.
:Umemwambia uongo ili amchukie baba yake. Inawezekana pia wewe unamchukia baba yako kwasababu mama yako alikudanganya, mama yako alikufanya umuone baba yako mbaya. Sasa naona wewe pia umeamua kunifanyia hivyo kwa mwanangu. Si ndio (kwa hasira)
Mr Moses akasimama akiwa amempa mgongo Joyce kisha akachomoa bastora. Akageuka kumtazama Joyce…
Mr Moses: Nieleze nini ambacho sikijui? (akiwa amshika bastora mkononi)
Madam Joyce Akaanza kulia…
Joyce: Upo sawa Moses, upo sawa... Hukutaka kunipa nafasi kukueleza ukweli, sawa mi nipo tayari niuwe.
Mr Moses: Nambie (akamnyoshea bastora)
Joyce: Ni kweli kuna siku Eva alikuja kuniuliza: Mama vyote alivyo niambia baba wa kambo ni vya kweli nikamjibu ndio ila sikujua alimwambia nini.
: Nakumbuka kabla Eva hajaniuliza, alikuja kwanza Damian akaniambia.
KUMBUKUMBU
Damian: Eva kaniuliza maswali mengi kuhusu wewe na Mr Moses.
Joyce: Kuhusu nini tena?
Damian: Ety!! Ananiambia baba na mama wananidanganya wanawezaje kuachana kwa amani bila kukosana.
Joyce: Eehh!! Umemjibu nini?
Damian: Nimejitahidi kumuelewesha vizuri, nikamwambia baba na mama waliachana vizuri bila kuwa na shida yoyote.
Joyce: Woow! umemuelewesha vizuri kwasababu ni kweli tuliachana vizuri bila ugomvi.
Damian: lakini kunakitu nataka nikuombe.
Joyce: Mmhuu!! sawa usijari.
Damian: Eva akikuliza akitaka kujua kama ni vya kweli nilivyo muambia? Mjibu ndio ni vya kweli.
Joyce: kwanini nimjibu hivyo? Ikiwa ulivyomuambia vyote ni vya kweli.
Damian: Oooh! usiwaze ni jambo jema, Nataka Eva atuamini na sisi kama ambvyo anamuamini baba yake ili asiwe anaogopa kutueleza shida zake na sisi tumtatulie kama wazazi wake.
Joyce: Ni hivyo tu, basi hamna shida nitamuambia.
MWISHO WA KUMBUKUMBU
Joyce: Siku iliyofata Eva alinifata na kuniuliza nikamjibu nikiwa naamini alichomwambia baba yake wa kambo ni kizuri.
: Lakini baadae nilijua baba yake wa kambo alimdanganya baada ya kumuona Eva anamawasiliano mabaya na wewe. Nilimfata Eva nikamuuliza nini kimesababisha amchukie baba yake.
KUMBUKUMBU
Joyce: Eva mwanangu!! Mbona sikuhizi hutaki kuongea na baba yako?
Eva: Sipendi, kwasababu simpendi.
Joyce: Humpendi!! (kwa mshangao)
Eva: Ndio namchukia sana baba, sijui hata!! kwanini alikua baba yangu… Siwezi kumpenda baba ambae alikuwa anamtesa mama yangu, anamnyanyasa, anampiga kisha akampa talaka mama ili akae mbali na mtoto wake. Baba kanifanya nikae mbali na mama yangu.
Joyce: Evaa!! Nani kakuambia hayo? (kwa mshangao)
Eva: Anae nipenda, anae nijari baba yangu wa kweli, alieniambia ni baba yangu wa kambo na ahidi mbele yako nitampenda yeye pamoj na wewe mama yangu tu, na yoyote atakae wakosea nyinyi kanikosea mimi.
Joyce: lakini…!!
Kabla sijamuambia chochote nikasikia sauti ya baba yake wa kambo akimuita Eva.
Damian: Eva mwanangu… Uko wapi twende tukatembee.
Eva: Naam baba!! nakuja baba yangu kipenzi.
Baada ya hapo Eva hakutaka kunisikiliza akaondoka...
Eva: Mama byee ngoja niwahi baba atakua tayari amefika kwenye gari.. Tutaongea badae bye mwaaah!! (Akaondoka)
MWISHO KUMBUKUMBU
Joyce: Baada ya hapo nikabaki sina cha kusema zaidi kujiuliza maswali mwenyewe, nikajua shida iliyopelekea Eva kuwa na mawasiliano mabaya na wewe. Ulivyo nitafuta unataka tukutane nikaona ndio itakuwa wakati mzuri wa kukuambia haya yote ili tujue tunamsaidiaje mtoto wetu.
: Lakini nafika hapa unanilaumu mimi tu, ndio ni sahihi Moses mimi ndio mwenye kosa, yaani hata mimi kuachana na wewe ni kwa ujinga wangu kukubali ushawishi wa Damian. (akiwa analia)
Mr Moses: Usilie Joy, ni kawaida inatokea katika maisha… Nisamehe mimi pia, sikujua haya yote.
Joyce: Siwezi kukusamehe Moses kwasababu hauna kosa, mimi ndio mwenye makosa.
Mr Moses: Sawa Joyce, lakini umeshamjua mbaya inabidi uwenae makini, pengine yupo kwako kwajiri ya mali zako.. Inabidi uwe makini, usi-saini nyalaka yoyote atakayo kuletea bila kuisoma vizuri, sawa.
Joyce: Sawa Moses nimekuelewa, lakini mimi sahivi sihitaji kuwanae. Yani!! simpendi, siwezi kuishi na mtu wa namna hii.
Mr Moses: Inabidi uwe mvumilivu, maana sahivi ukisema uachanenae mtagawana mali kwasababu mmefunga ndoa.
Joyce: Sasa tufanyaje Moses.
Mr Moses: Saivi ambacho hatakiwi kujua ni kwamba mimi na wewe tuna mawasiliano mazuri, inatakiwa aendele kujua sisi ni maadui. Yaani ikibidi igiza kama unanichukia sawa.
Joyce: Sijui kama nitaweza ila nitajitahidi.
Madam Joyce akampigia magoti Mr Moses akimuomba msamaha.
Joyce: Moses naomba unisamehe kwa yote niliyo kutendea.
Kabla Mr Moses hajamjibu… Ghafla iliasikika sauti
Eva: Weeeee!! muache mama yangu, walinzi mkamateni huyo.. (sauti ya juu kwa hasira)
*** ITAENDELEA ***
Comments (6)
See all