Please note that Tapas no longer supports Internet Explorer.
We recommend upgrading to the latest Microsoft Edge, Google Chrome, or Firefox.
Home
Comics
Novels
Community
Mature
More
Help Discord Forums Newsfeed Contact Merch Shop
Publish
Home
Comics
Novels
Community
Mature
More
Help Discord Forums Newsfeed Contact Merch Shop
__anonymous__
__anonymous__
0
  • Publish
  • Ink shop
  • Redeem code
  • Settings
  • Log out

FATHER & DAUGHTER (Swahili)

MAMA BORA

MAMA BORA

Sep 28, 2022


...

Eva: Weee!! muache mama yangu, walinzi mkamateni huyo... (sauti ya juu kwa hasira)

Mr Moses baada ya kuona wanakuja kumkamata akakimbia, walinzi walimfukuzia lakini hawakumpata, walifanikiwa kumjeruhi kumpiga risasi ya kwenye bega la kulia.

Eva: Mama upo salama, hajakumiza nimemuona ameshika bastora. (kwa hofu)

Joyce: Hapana hajanidhuru, niambie mmejuaje kama nipo hapa?

Damian: Tumekupata kupitia mfumo wa GPS uliyofungwa kwenye gari yako.

Joyce: Ooh!! ok sawa, asanteni kwa kuniokoa.

Joyce akaficha ili wasijue kama sahivi wanamahusiano mazuri na Mr Moses. Wakamchukua Madam Joyce wakaondoka pamoja mpaka kwenye gari, wakaingiza ndani ya gari. Lakini Damian na Eva walikua bado hawajaingia kwenye gari wapo nje.

Eva: Kama vile ulijua ukasema tumfate mama, inamaana bado anataka kumua mama.

Damian: Sahivi inabidi tuwe makini sana anaweza kutuangamiza wote. Shika hii itakusaidia kujilinda akitaka kukudhuru (akampa bastora), ila usimwambie mama maana hataki utumie hii ukiwa na umri huu. Pia kumbuka zimebaki risasi nne tu tumia vizuri kwa makini, ukilenga hakikisha haukosi.

            : Aya Eva ngoja mimi nitangulie na mama yako, naona hajisikii vizuri.

Kabla hajaondoka Eva akamuangalia baba yake wa kambo kisha akamuita.

Eva: Baba. (kwa sauti ya upendo)

 Mr Damian akageuka.

Eva: Asante.

Mr Damian Akatabasamu kisha akaingia kwenye gari wakaondoka. Muda huo wale walinzi wawili wanarudi wanamkuta Eva.

Eva: Vipi mmemkosa?

Bodygaurd-1: Ndio madam, lakini tumefanikiwa kumpiga risasi ya bega.

Eva: Vizuri hicho kidogo kinamtosha kwa sasa, naomba siku nyingine muwe makini hakikisheni mnamrinda mama na baba, sawa.

Bodyguard-2: Sawa boss. 

NYUMBANI KWA MR MOSES

Mr Moses anarudi nyumbani kwake anashuka kwenye gari akiwa anachechemea, anataka kuanguka lakini anashikwa mkono na mfanyakazi wake anamsaidia kuingia ndani.

Mr Moses: Muite Dr Elia aje anifanyie matibabu.

Mfanyakazi-bustani: Sawa bosi nitafanya haraka iwezekanavyo.

Dr Elia ni mzee apatae miaka 60 anakuja anamfanyia matibabu anaitoa risasi huku wakiendelea na mazungumzo.

Dr Elia: Kunatatizo gana tena bwana Musa.

Mr Moses: Nilivamiwa na wezi, walitaka waniibie (Akaficha ili asijue kinachoendelea)

Dr Elia: Oohh!! pole sana kijana wangu, lakini inatakiwa na wewe ujiwekee usalama zaidi inawezekana sio wezi ila ni hao washindani wako wa biashara wanataka wakuangamize, tumesikia habari ya uongo waliyokuzushia kuhusu wewe kuachana na mke wako Joyce. Wakati sisi ukweli tunaujua mliachana kwa amani kabisa na wewe huna kosa lolote.

Mr Moses: Yeah!! kweli kwa mtu ambae hajaishi kwenye nyumba hii hawezi kujua, mnaojua ni nyinyi ambao mnakaa humu.

Dr Elia: Ni kweli kijana wangu, mimi nawaombea muwe na mwisho mzuri maana mlipendana kweli.

Mr. Moses: Natamani pia iwe hivyo mzee wangu.

Dr Elia: Sawa boss wangu, bahati nzuri risasi haijafika kwenye mfupa, sasa unatakiwa uendelee kutumia hizi dawa utapona.

Mr Moses na dr Elia wakagana kila mtu akaendelea na mambo yake. Mr Moses akaingia chumbani kwake akakaa kwenye kiti pembeni kidogo ya kitanda akaweka bastora yake kwenye meza kisha akachukua grasi akamimina kinywaji na kuanza kunywa taratibu, kichwani akiwa na mawazo mengi huku akiangalia picha ya binti yake Eva iliyokuwa mezani.

SIKU ILIYOFATA

Katika kampuni ya madam Joyce ( JOY ) wafanyakizi wakiendelea na kazi zao, tunamuona Damian akiwa kazini akikagua toleo lao jipya la nguo.

Damian: Wooow!! Hii itakuwa kari kuliko ile ya Mr Moses na kampuni yake ya PROUD.

Wakati akiendelea kukagua simu yake ikaita, akasogea pembeni kuongea na simu.

Damian: Hallo!!

Simu: Eeeh!! hallo vipi bado tu maana mi nimechoka kuvumilia.

Damian: Unachoka vipi sasa wakati ndio nipo hatua za mwisho mwisho, yaani imebaki kidogo tu anikabidhi miliki ya kampuni hii na kizuri zaidi tunaweza kuchukua na ile kampuni nyingine.

Simu: Kivipi?

Damian: Nimefatilia nimegundua Eva ana-hisa katika kampuni ya baba yake.

Simu: Ok sawa ila uwe makini, maana mi nimeshamaliza kazi yangu bado nakusubiri wewe tu, naona pia unataka unizunguke sijui umenogewa na mapenzi mpaka umenisahau mimi, lakini kumbuka nimetoa jasho langu kwenye hili jambo.

Damian: Sawa usijari nitakamilisha mpenzi wangu na kampuni moja itakuwa yangu moja yako hahaha!! (kwa hofu)

Simu: Aya sawa ila mimi sikuelewi kabisa.

kipindi Damian anaongea na simu madam Joyce alikua pembeni amejificha anasikiliza yote aliyokua anaongea.

Joyce: Sasa alikua anaongea na nani tena kuhusu maswala ya kuchukua kampuni. (akawaza)

Baada ya Damian kumaliza kuongea na simu madam joyce akamfata.

Joyce: Umemaliza kukagua toleo letu jipya.

Damian: Ndio naona yetu itakuwa bora zaidi kuliko toleo la Mr Moses.

Joyce: Ndio!! itabidi tuonyeshe kuwa sisi tuko bora zaidi yao.

Damian: Yeah!! Hii itavunja rekodi ya mauzo mke wangu.

Joyce: Okay !! Sorry, niazime simu yako niongee na Eva, simu yangu inazingua.

Damian akampa simu yake Joyce lakini hakumfatilia kwasababu wakati huo wandishi wa habari walikua wamefika eneolile kwajili ya kurusha matangazo ya uzinduzi wa toleo jipya la nguo kwahiyo Damian hakumfatilia Madam Joyce akawa bize na waandishi wa habari. Madam Joyce akasogea pembeni akaingia call history akainakiri ile namba akaitunza kwenye simu yake kisha akamrudishia simu Damian wakati bado akiwa anaongea na waandishi wa habari.

Madam Joyce akaingia ofisini kwake akachukua mkoba wake kisha akamwachia maagizo mfanyakazi (Mr Damian akimaliza kuongea na waandishi wa habari utamwambia nimeenda kumchukua Eva). Kisha akaingia kwenye gari wakati huo Damian akiwa anaongea na waandishi wa habari.

Madam Joyce alipofika nyumabani kwake akachukua kompyuta yake akaunganisha na mtandao kisha akanza kuifatilia ile namba kupitia mitandao ya kijamii mpaka akaipata sura harisi ya miliki wa namba hiyo.

Joyce: Oooohh!! Mungu wangu. Ok sasa nimekufahamu zaidi mpumbavu wewe..!

         : Sasa ni muda sahihi wa kumuambia Eva ukweli, lakini kabla ya kuongea na Eva itabidi nikutane na Moses nimuambie kuhusu hili. Oooh!! Mungu nisamehe sikujua hili mapema.

Mmiliki wa namba hiyo alikua ni mwanamke. Na inaonekan sio mgeni kwa Madam Joyce.

*** ITAENDELEA ***

custom banner
petercharlz255
BOBOtheBEST-Comics

Creator

YALIYOMO KWENYE EPISODE IJAYO (EP 07)
...
Damian: Hey!! Madam yukowapi?

Mfanyakazi-Sekretali: Ameondoka amenambia nikutarifu anaenda kumfata Eva.

Damian: Oooh11 mbona...
...

Lakini ghafla rafiki yake alishikwa na butwaa.

Rafiki: Eva Eva!! Ona hii habari…!!

Eva: Ni kampuni ya mama yangu, gari iliyo...
...

Joyce: Hallo!!

Mfanyakazi: Hallo! madam njoo ofisini haraka kunatatizo limetokea, kunam...

Joyce: Ety Nini!!, Damian ame...
...

Eva: Baba baba, uko salama baba yangu?

Damian: ...

...

Joyce: Nani sasa amefanya hivi?

Damian: Bado sijajua Joyce.

Eva: Mimi namfahamu..!! (Kwa hasira)
...

Damian: Hey! unaweza kuendesha gari vizuri?

Dereva-Tax: Ndio mzee.

Damian: Ok shika hii hela wafukuzie wale.
...

USIKOSE EPISODE IJAYO

#fatheranddaghter #bobothebestcomics #bobothebeststudios #petercharlz255

Comments (1)

See all
Edu sal
Edu sal

Top comment

Nice

1

Add a comment

Recommendation for you

  • Secunda

    Recommendation

    Secunda

    Romance Fantasy 43.3k likes

  • Invisible Boy

    Recommendation

    Invisible Boy

    LGBTQ+ 11.4k likes

  • What Makes a Monster

    Recommendation

    What Makes a Monster

    BL 75.3k likes

  • Silence | book 1

    Recommendation

    Silence | book 1

    LGBTQ+ 27.2k likes

  • For the Light

    Recommendation

    For the Light

    GL 19.1k likes

  • Silence | book 2

    Recommendation

    Silence | book 2

    LGBTQ+ 32.3k likes

  • feeling lucky

    Feeling lucky

    Random series you may like

FATHER & DAUGHTER  (Swahili)
FATHER & DAUGHTER (Swahili)

1.6k views5 subscribers

Mr Moses katika maisha yake yote licha ya kuwa na utajiri mkubwa lakini kuna kitu kimoja anakipenda kuliko vitu vyote. Mr Moses anampenda binti yake (Eva) kuliko mtu yoyote kuliko kitu chochote kwenye hii dunia yenye mabilioni ya watu na vitu. Lakini anajikuta anaingia kwenye wakati mgumu baada ya binti yake Eva Moses anapobadilikaka na kuwa adui yake mkubwa...
Subscribe

8 episodes

MAMA BORA

MAMA BORA

135 views 3 likes 1 comment


Style
More
Like
List
Comment

Prev
Next

Full
Exit
3
1
Prev
Next