UPANDE WA OFISI ZA JOY
Damian amemaliza kuongea na waandishi wa habari baada ya kuzindua toleo jipya la nguo.
Damian: Hey!! Madam yukowapi?
Mfanyakazi-Sekretali: Madam ameondoka amenambia nikutarifu anaenda kumfata Eva.
Damian: Oooh!! mbona hajanisubiri.
:Ngoja nami nimfate (akawaza)
Damian akatoka ofisini na kuelekea eneo alipopaki gari yake ( parking ) lakini kwa bahati nzuri kabla hajafika kwenye gari yake, gari ililipuka na kumrusha mbali kama mita 10 kutoka eneo ilipokuwa gari, alijeruhiwa kidogi na vipande vya moto vilivyoruka baada ya mlipuko wa bomu pia aliumia baada ya kutua vibaya aliporushwa na bomu. Waandishi wa habari waliokuwa maeneo hayo wakaripoti tukio hilo.
CHUO KIKUU (UDSM)
Eva akiwa anatoka chuo yeye pamoja na rafiki zake, akiwa anawasubiria wazazi wake wampitie.
Eva: Wooow!! leo nimefurahi sana, vazi letu kuchaguliwa kuwa namba moja.
Rafiki: Yaani! hii itabidi i-trend lazima niweke kwenye mitandao tupate maoni pia.
Lakini ghafla rafiki yake alishikwa na butwaa.
Rafiki: Mungu wangu Eva, Eva!! angalia hii habari…!!
Eva: Hii ni kampuni ya mama yangu, gari iliyolipuka ni gari ya baba yangu wa kambo.
Eva ikabidi achukua usafiri haraka awai kwenda eneo la tukio.
Eva: Chidy unaweza kuniazima pikipiki yako…?
Chidy: Leo imekuaje mtoto wakishua unaniomba pikipiki!!?
Eva: Ok poa niambie itagharimu shingapi?
Chidy: Hayo ndio maneno, nipe mkono.
Eva: Ok chukua hii 60.
Eva akachukua pikipiki akaondoka haraka kuwai eneo la tukio.
NYUMBANI KWA MADAM JOYCE.
Madam Joyce anapigiwa simu na mfanyakazi wa kampuni yake.
Joyce: Haloo!!
Mfanya: Haloo! madam njoo haraka ofisini kunatatizo limetokea, kunamripuko, gari ya boss Damian imeripuka.
Joyce: Eti Nini!!, Damian amepona!
Simu ikakata Joyce akangia mtandaoni kuangalia habari akakuta mitandaon imeenea habari hiyo tu. Haraka haraka akaeleke eneo la tukio.
OFISI ZA JOY
Eva amefika katika ofisi za mama yake anakuta watu wamejaa Polisi na zimamoto wameshafika pia anamkuta baba yake wa kambo yupo pembeni na watu wa huduma ya kwanza.
Eva: Baba baba, uko salama baba yangu?
Damian: Ndio nipo salama Eva, nimejeruhiwa kidogo tu.
Eva: Vipi mama yeye yuko wapi? Je yupo salama?
Damian: Ndio mama yako alitangulia kukufata itakuwa umepishana nae.
Eva: Pole sana baba yangu... (akiwa analia)
Madam Joyce pia akafika eneo la tukio.
Joyce: Damian uko salama!?
Damian: Ndio niko salama Joyce.
Joyce: Shida nini!? gari ilikua na shida gani!
Damian: Mripuko wa bomu.
Joyce: Bomu!!?
Damian: Ndio wataramu wamesema hilo ni bomu la kutega na sio mlipuko wa mafuta.
Joyce: Nani sasa amefanya hivi?
Damian: Bado sijajua Joyce.
Eva: Mimi namfahamu..!! (Kwa hasira)
Eva akaondoka eneo lile akiwa na hasira akachukua pikipiki aliyokujanayo akawasha na kuondoka huku mama yake
Joyce: Evaaa subiri, unaenda wapi wewe, mwanangu nisubiri.. Acha kufanya hicho unachotaka kufanya. Evaaa!!
Madam Joyce na yeye pia akachukua gari yake na kuanza kumfukuzia Eva, Damian pia akawasukuma madaktari akachukua usafiri.
Damian: Hey! unaweza kuendesha gari vizuri?
Dereva-Tax: Ndio mzee.
Damian: Ok shika hii hela wafukuzie wale.
Damian akaingia kwenye gari na kuwafukuzia. Eva alikua na hasira sana akafika katika ofisi za PROUD akashuka kwenye pikipiki kisha akaingia ndani ya geti mlinzi moja akataka kumzuia lakini mlinzi mwingine aliekua amekaa pembeni anakula (bonge) akamwimbia.
Mlinzi1: Hey! Hey! madam simama, fata utaratibu wa kuingia ndani.
Mlinzi (Bonge): Wewe huyo ni mtoto wa boss usirudie kumzuia, huyo ni boss wako.
Mlinzi1: Mmmhh!
Eva akaingia ndani ya ofisi akiwa na hasira baadhi ya wafanyakazi wanao mfahamu wanamsalimia lakini hawajibu wanabaki wanashangaa!! Eva akaingia kwenye lifti kuelekea kwenye ofisi ya baba yake. Akabonyeza rimoti impeleke ghorofa ya 43.
Wakati huo Madam Joyce na yeye pia anafika katika ofisi za PROUD mlinzi anataka kumzuia.
Mlinzi1: Hey! Hey! madam simama, fata utaratibu tafadhali?
Mlinzi (bonge): wewe huyo ni mke wa boss. Unamzuia boss wako asingie ofisini mara ya tatu utafukuzwa kazi.
Mlinzi1: Aaaahhhg!!
Miss pia akaingia ofisini akiwa anakimbia kumuwai Eva wafanyakazi wakabaki na mshangao. Madam Joyce akaingia kwenye lifti pia akabonyeza namba 43. Wakati huo Damian na yeye anafika katika ofisi za PROUD. Akashuka kwenye gari akaingia ndani lakini mlinzi hakumzuia.
Mlinzi1: Mmmh!!?
Mlinzi (bonge): Vipi wewe mbona hujamzuia huyoo!! anaingia bila kufata utaratibu.
Mlinzi1: Oooh! vipi huyo sio muhusika hapa, sio shemeji yake boss au mjomba au rafiki yake boss!?
Mlinzi(bonge): Mkamate wewe huyo mzuie. Huyo sio muhusika hapa.
Walinzi wakaanza kumkimbiza Damian lakini alikua amewacha mbali akawai kufika kwenye lifti. Kutokana na kuwa mgeni kwenye ofisi zile hakujua Mr Moses anapatikana ghorofa ya ngapi hivyo akabonye namba 40. Wafanyakazi wakabaki na mshangao wasijue nini kinaendelea!
Wlinzi1: Wewe simamaa.
UPANDE WA EVA
Eva anaingia katika ofisi ya baba yake anamkuta baba yake kasimama akiwa anangalia nnje upande wa kioo akiwa na mawazo sana. Eva anachomoa bastora kisha akanyosha kuelekea kwa baba yake (akamnyoshea).
Eva: Babaaaa..!!
Moses anageuka kwa mshtuko anashangaa kumona Eva amemnyoshea bastora huku akitokwa na machozi.
Mr Moses: Please!! Eva usifanye hivyo!!
*** ITAENDELEA *** - Jumatatu 3 October 2022
Comments (2)
See all