...
UPANDE WA EVA
Eva anaingia katika ofisi ya baba yake anamkuta baba yake kasimama akiwa anangalia nnje upande wa kioo akiwa na mawazo sana. Eva anachomoa bastora kisha akanyosha kuelekea kwa baba yake (akamnyoshea).
Eva: Babaaaa..!!
Moses anageuka kwa mshtuko anashangaa kumona Eva amemnyoshea bastora huku akitokwa na machozi.
Mr Moses: Please!! Eva usifanye hivyo!!
Eva: Baba nilikuambia nini kuhusu familia yangu, nilikuambia nini kuhusu kumdhuru mama au baba yangu, mara mbili zote unataka kuwaua wazazi wangu, mara ya kwanza mama na sahivi baba yangu.
Mr Moses akataka kusogea, akapiga hatua moja lakini Eva akampiga risasi moja kwenye mguu wa kulia. Madam Joyce akaisikia sauti ya bunduki baada ya Eva kufyatua risasi, ikamlazimu aongeze mwendo kwenda kumzuia Eva.
Eva: Usinisogelee!! Nijibu kwanini unataka kuwaua wazazi wangu!?
Mr Moses: Oohh!! Eva mimi baba yako nakupenda, nampenda mama yako na baba yako pia. Nielewe sijafanya kitu chochote kibaya kwa wazazi wako. Nielewe Eva wewe ndio kila kitu kwangu.
Eva: Baba wewe muongoo. (kwa uchungu)
Wakati huo Joyce amefika mlangoni akaingia ndani, wakati anaingia akafunga kitasa cha mlango akaweka loki kabisa. Huku Eva akamnyoshea bastora baba yake.
Joyce: Evaaa hapanaaaa, Evaaaaa!!!
Lakini Madam Joyce alikua amechelewa Eva akafyatua risasi ikampiga baba yake maeneo ya kifuani upande wa kushoto eneo karibu na moyo, Moses akanguka chini, baada ya kumpiga risasi baba yake kwa mshangao na hofu Eva akangusha bastora chini Madam Joyce akakimbia na kumshika Mr Moses pale chini.
Mr Moses: Nakupenda Joyce nakupenda wewe na Eva. ( Moses akafa )
Joyce: Mozeee!! Usiniache Moses unaniachaje mimi bado nakuhitaji, usiniache uliniahidi utakuwa na mimi hutoniacha inawezekanaje leo... (Akiwa analia)
Evaa akabaki anashangaa kuona mama yake anamlilia baba yake kwa uchungu na mapenzi ya dhati, alishiwa nguvu akapiga magoti chini.
Eva: Mama nambie ukweli maana mi' sielewi.!!
Joyce: Usijalaumu mwanangu sio baba yako wala wewe mwenye makosa lakini mimi ndie mwenye makosa.
Upande Mr Damian bado anaangaika kufika katika ofisi ya Mr Moses kwasababu hakujua ofisi zinapatiakana ghorofa ya ngapi, bado anakimbizana na walinzi alishuka ghorofa ya tatu kabla ya kufika ofisi ya Mr Moses ikabidi aanze kutumia njia ya ngazi.
Joyce: Mimi na baba yako tulipendana sana, na hatukujua kama siku moja tutakuja kuachana na kusababisha matatizo kiasi hiki, lakini kwa bahati mbaya wewe hukuona kwasababu ulikua mtoto mdogo sana.
: Tuliishi kwa kupendana na kwa pamoja tulifanya kazi katika kampuni yetu ya PROUD mpaka pale ilipotokea ugomvi.
Eva: Ugomvi ulisbabishwa na nini?
Mam: Kipindi kampuni yetu inakua watu wengi walijiunga na kampuni yetu, wanaume kwa wanawake na kipindi kile kampuni yetu ilikua na unashindani sana na kampuni ya HIGH CLASS iliyokuwa inamilikiwa na Mr Daminan. Lakini sisi tulikua juu kutokana na ubora wa bidhaa zetu, Siku moja tulipata amfanyakazi wa kike jina lake Vivian, Na kipindi hicho wewe ulikuwa mdogo sana ikabidi mimi nijihusishe na mambo ya kifamilia na nikapunguza majukumu ya kiofisi sasa mfanyakazi yule ikabidi achukue nafasi yangu...
: Hapo ndipo ugomvi ulipoanza. Baba yako alikua akichelewa kurudi nyumbani, akawa bize na kazi na muda wote alikuwa na yule mwanamke mimi bila kufikiria pia wakati nikiwa kazini nilikua bize kama baba yako nikashikwa na wivu na hapo tukaanza kukosana na baba yako.Yule mwanamke alipogundua akaanza kutumia hali hiyo kutimiza haja yake. Alianza kujingiza kwenye mapenzi na baba yako licha ya baba yako hakumuhitaji, alimuwekea mitego na kilakituko ili tu ampate.
:Sasa wakati huo Mr Damian akanifata na kuniletea ushahidi wa kila aina, akinionyesha baba yako anamahusiano na yule mwanamke... Mwanzoni ilikua vigumu kuamini lakini kadili muda ulivyozidi kwenda na mimi ninavyo mpenda baba yako nikaanza kuamini. Ikafika kipindi tukawa tunakosana kila siku na baba yako, hali hii ilidumu kwa muda wa mwaka mmoja mpaka ikafikia hatua baba akamfukuza kazi yule mwanamke lakini haikuwezekana kuwa pamoja na baba yako tena licha ya kumfukuza yule mwanamke. Kwasababu alichelewa, mimi pia nilijikuta nimeingia kwenye penzi na Mr Damian.
:Nilikua nikilipiza kisasi kwa baba yako, kisasi ambacho sikujua sio cha kweli, baba yako akamfukuza yule mwanamke lakini mimi bado niliomba taraka na tukaachana na baba yako amabae alibaki na wewe. Tukagawana hisa za kampuni mimi nikaanzisha kampuni mpya y JOY nikiwa na Mr Damian ambayo tumekuwa tukishindana na kampuni ya baba yako kwa miaka 13 sasa. Lakini muda wote tangu tuachane na baba yako hajawai kuoa mwanamke mwingine akiamini kwenye maisha yake tayari amepata kilakitu,kila kitu ambaye ni wewe… Wewe ndie ulikua kilakitu kwake.
Eva: Mama…!! Yule mwanamke ni nani? Na kwanini alikuja kuharibu ndoa yenu!?
Mam: Leo ndio nimegundua yule mwanamke ni nani.
Eva: Ni nani?
Mam: Leo ndio nimegundua yule mwanamke ni mke wa baba yako wa kambo. Nilimsikia Damian akiongea na simu nikamsikiliza kwa makini na katika mazungumzo yake nikagundua lengo lao ni kuchukua umiliki wa kampuni zote mbili. Damian anataka achukue miliki zote za kampuni yangu na pia nimesikia akisema amegundua wewe pia una hisa kwenye kampuni ya baba yako kwahiyo ukaribu aliotengeneza na wewe ili achukue mali zako pia.
Eva: Umejua vipi kama mwanamke anae ongeanae ndio yule.
Joyce: Baada ya Damian kumaliza kuongea na simu nilimuomba simu yake ili nipate nafasi ya kuichukua namba ya mtu aliyekuwa anawasiliana nae, kwa bahati nzuri nikafanikiwa kisha nikaifanyia uchunguzi namba ile kujua ya nani... Ndio nikagundua ni ya yule mwanamke, mke wa baba yako wa kambo. Na wakati huo nikataka nije nimtarifu Mr Moses. Nije nimwambie kitu nilichogundua, chanzo cha ugomvi wangu na yeye na ni nani hasa kasababisha, nimwambie kuwa adui yetu ni Mr Damian lakini sina bahati nimeshindwa Moses amekufa (akalia)
Eva: Nisamehe mimi mamaaa!! (akilia), sikujua ninacho kifanya, nime toa maisha ya baba yangu, mimi ambae ndio kilakitu kwake, baba amesalitiwa na wote aliowapenda, wakwanza mke wake na sasa mtoto wake… Nimefanya nini sasa hiki, nimefanya nini mimi. (akilia)
Wakati huo Damian amefanikiwa kufika katika ofisi za Mr Moses, anajaribu kufungua mlango lakini anashindwa kwasababu kipindi Joyce anaingia aliufunga kwa ndani. Walinzi wakiwa nyuma wanamfukuzia.
Damian: Oooh!! nini hiki, mlango umefungwa.
: Eva , Joyce ni mimi Damian nifungulie. (akigonga mlango)
Kimya hakuna aliemjibu.
Mlinzi1: Hey!! Simama hapo hapo, jisalimishe mwenyewe.
Mlinzi(bonge): Simama bana!! Mambo gani haya unatukimbiza kama watoto. (Amechoka akiwa ameshika magoti)
Damian: (Akanyosha mikono juu) Sawa ninajisalimisha, lakini nisikilizeni boss wenu itakua amepatwa na tatizo humu ndani maana nagonga mlango lakini hafungui wala hakuna anaenijibu.
Mlinzi1: Hiyo haijarishi, tunacho hitaji tukutoe humu ndani.
Mlinzi(bonge): Boss yupo na mambo ya familia wewe hayakuhusu. (Amekaa chini hoi)
Wakati huo Eva na mama yake wapo ndani walisikia mlango unagongwa lakini hawakujua nani wala hawakujari maana wote hawaelewi. Joyce akachukua ile bastora iliyokuwa pale chini.
Eva: Mama unataka ufanye nini!?
Joyce: Eva, Baba yako alistahiri kuishi sio mimi, lakini nitawezaje kuishi bila yeye tena? Itawezekanaje mimi kuishi wakati ndie mwenye makosa... (Joyce akaweka bastora kichwani)
Eva akataka kuwai lakini Joyce akafyatua risasi ikazama kwenye kichwa mpaka ikatokea upande wa pili na ikapelekea kifo kwa Joyce.
Eva: Mamaaaa….!!? hapana!
Walinzi pamoja na Damian walisikia ule mlio wa risasi. Wakabaki na mshangao…
Damian: Si mnaona niliwaambia, kunatatizo humu.
Mlinzi(bonge): Fanya haraka tuvunje huo mlango!!
Wakachukua mtungi wa gesi uliokuwa umeninginia pembeni kwenye ukuta na kuanza kuvunja mlango. Wakati huo mlinzi1 anapiga simu kituo cha polisi kuripoti tukio hilo.
Mlinzi1: hallo!! kutoka katika ofisi za PROUD naripoti kunatukio la uharifu linafanyika…!!
Simu: Sawa tunafika sasa hivi hapo.
Kule ndani Eva akiwa amewashika baba yake pamoja na mama yake huku analia.
Eva: Baba hapanaaa Mama hapanaaa…!!
Damian na walinzi wanafanikiwa kuvunja ule mlango na kuingia ndani, wanamkuta Eva analia akiwa amewashika wazazi wake, Kila mtu akiwa anashangaa Damian anaogopa kumsogelea Eva anasimama mbali kidogo karibu na dirisha lililojengwa kwa kioo kuanzia kwenye sakafu mpaka kwenye paa.
Damian: Eva uko salama!?
Lakini Eva hakumjibu chochote.
Damian: Eva nini kimetokea mwanangu!?
Eva amekaa kimya anatokwa na machozi tu, Damian kumuangalia Eva mkononi ameshika bastora.
Damian: (Akawaza) Inawezekana Eva kaujua ukweli nini!! Mbona hanijibu!?
Eva akamuangalia kwa hasira baba yake wa kambo.
Damian: Eva, usijari kilakitu kitaenda sawa mwanangu mimi baba yako nipo hapa. ( kwa uoga)
Wale walinzi wameshindwa kumsogelea maana ameshika bastora…
Mlinzi1: Vipi tunafanyaje!?
Mlinzi(bonge): Tusikilizie labda atamsikiliza baba yake mlezi, tusi-force anaweza akafyatua nyingine!!
Mlinzi1: Sawa.
Damian akaona Eva haeleweki akataka achomoe bastora yake ili ajihami maana inaonekana Eva amegundua. Ile kwa haraka anataka achomoe bastora Eva alikuwa haraka zaidi akampiga risasi maeneo ya kifua huku Damian bastora alioshika ikafyatua risasi lakini kutokana na msukumo wa risasi iliyompiga kifuani risasi yake ilipoteza muelekeo ikapiga kioo na kukitoboa, Damian akaangukia kile kioo na kukivunja, akaanguka kutoka ghorofa ya 43 mpaka chini akatua juu ya gari iliyokuwa imepaki pale nje na kupoteza maisha…
Eva: Ulisema kweli!! Unapo lenga kuwa makini, usipoteze shabaha. Nimefanya hivyo Damian.
Eva baada ya kufanya hivyo akaiweka bastora kichwani kwake akitaka ajiue lakini kupiga risasi zilikua zimeisha...
Eva: Oooh hapana!! zilikua nne tu.
Wakati huo polisi walikua wamefika eneo la tukio, wakamchukua Eva pamoja na miili ya baba (Mr Moses) na mama (Joyce) yake pamoja na mwili wa Damian kwajili ya uchunguzi zaidi... Wakati wanatoka katika zile ofisi, nje palikuwa na waandishi wengi wa habari, Eva na baadhi ya mashahidi wakachukuliwa lakini kabla hawajaondoka mkuu wa polisi analetewa taarifa…
Polisi: Mkuu, tumefanikiwa kumfahamu mtu alieweka Bomu kwenye gari ya Mr Damian.
Polisi (mkuu): OK!! chukua kikosi mara moja mkamateni, pengine anaweza pia akawa muhusika wa tukio hili, jitahidi mlete akiwa mzima anaweza kutusaidi maana mpaka sahivi mimi sielewi.
Polisi: Sawa mkuu tutalitimiza hilo bila shaka.
Tunaona nchi nzima habari ni kuhusu tukio lililotokea kwenye ofisi za PROUD, na hapa kunamtu anaangalia TV, ni yule mwanamke ambae inasemekana ni mke wa Mr Damian.
TARIFA YA HABARI
Reporter: Nikiripoti kutoke eneo la tukio hapa katika ofisi za PROUD ambapo yamefanyika mauaji ya watu watatu wamiliki wa kampuni kubwa za uzalishaji wa nguo, wanaofahamika kwa majina Mr Moses miliki wa PROUD, Joyce miliki wa kampuni ya JOY pamoja na mume na mshirika wake Damian ambae muda mfupi alinusurika kufa kwa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari yake na muda mfupi mbele kufikwa na umauti kwa kupigwa risasi katika eneo hili la ofisi za PROUD. Huku muhusika mkuu akitajwa kuwa ni binti yao Eva Moses…
Vivian: Oohh! Sasa huu mwisho umekuaa mbaya zaidi!?
Wakati huo mlango wa chumba alichokuwa amekaa Vivian ulikua unagongwa, kwenda kufungua anakuta kundi la polisi kama kumi wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi, wote wamemnyoshea bunduki…
Polisi: Madam uko chini ya ulinzi (wakamvalisha pingu)
BAADA YA WIKI MBILI
Baada ya wiki mbili mbele, polisi wamechukua maelezo ya kutosha kwa Eva, na siku hiyo wamemuhitaji Eva kwenda kituo cha polisi kuwambia kama anamjua mwamke yule, akawaeleza polisi mwanamke yule ni nani, Lakini pia polisi wakamchukua yule mwanamke(Vivian) maelezo…
Polisi(Kitengo): Na kwanini sasa ulimtegea Bomu mumeo ilhali unajua yupo kwenye makubaliono yenu!?
Vivian: Nilihisi amenisaliti, amenizurumu maana ilikua muda mrefu sasa hajakamilisha mpango wetu na kila nikiongeanae hanipi majibu yaliyo sahihi ndio nikaamua kumtegea Bomu nimuue.
Polisi: kwahiyo unakili kuwa wewe ndio ulifanya tukio lile.
Vivian: Ndio ni Mimi nilifanya.
Siku zilienda ikafika siku ya kusomewa hukumu, Eva akiwa kizimbani.
Hakimu: kutokana na ushahidi tuliopata kwa muda mrefu sasa imengundulika kuwa Eva Moses hana hatia kufuatia shitaka lililokuwa linamkabiri la kufanya mauaji ya aliekua baba yake mlezi Bwana Damian… Ambopo mashahidi wawili (2) walinzi wa kampuni ya PROUD wanasema Eva alifanya tukio lile wakati akijirinda yeye asizulike na Bwana Damian ambae sasa ni marehemu. Na kwa mamlaka niliyopewa na serikeli ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nasema Eva yuko huru.
: Huku kwa mshtakiwa namba mbili 2 Bi Vivian anahukumiwa kifungi cha maisha jera kwakosa la kufanya jaribio la kumuua Bwana Damian kwa bomu, siku y tarehe… 2021. Pamoja na jaribio la kudhurumu kampuni za PROUD na JOY akishirikiana na aliekuwa mumewake Bwana Damian ambae kwasasa ni marehemu, majiribio yote hayo ambayo yalishindikana.
KESI IKAMALIZIKA HIVYO.
Baada ya kutimiza mika 18, mwanasheria wa baba yake mzazi pamoja na mwanasheria wa mama yake walimkabidhi nyalaka za haki miliki za kampuni pamoja na mali za wazazi wake, Eva alirudi shuleni kumalizia masomo yake na baadae akiwa na umri wa miaka 22 aliamua kuzivunja zile kampuni mbili na kutengeneza kampuni moja ambayo itatengeneza nguo zote za kiume na kike. Kampuni hiyo aliipa jina PJ akichukua herufi ya kwanza ya kampuni ya baba yake na herufi ya kwanza ya kampuni ya mama yake. Huku maana kuu aliyotizamia ni PLACE FOR JOY akimaanisha SEHEMU YA FURAHA. Kisha akawalika waandishi wa habari katika uzinduzi wa jina hilo jipya.
Eva: Ni miaka 5 sasa tangia kitokee kifo cha wazazi wangu ambao pia walikua wamiliki wa kampuni mbili shindani za mavazi ambayo ni PROUD pamoja JOY. Leo hapa tunaandika historia mpya kwa kuziunganisha kampuni hizi mbili na kuwa kampuni moja ambayo itaitwa PJ (PLACE FOR JOY), na sasa ni kampuni moja sio mbili tena... Lakini pia sahivi tutajihusisha na kuzarisha nguo za njinsia zote. Nakaribisha maswali…
Mwandishi: Asante sana Madam Eva !! Watu wanasema umewaua wazazi wako ili uchukue mali zao na zikufaidishe kwa mslahi yako.
Eva: Watu wanasema, na siwezi kuwazuia waache kusema, kwasababu hawajui mwanzo wa stori hii bali wanachokijua ni mwisho tu. Wanajua kuwa niliwaua wazazi wangu, lakini niwakumbushe baba yangu sahivi mnamuandika kama shujaa amekufa katika haki lakini vipi mnakumbuka mwanzoni mlimundika kama mnyanyasaji,katili,fisadi kwasababu mlikua hamjui mwanzo wa stori iliyopelekea mumpe majina hayo lakini mlivyoujua mwanzo mnamuita shujaa… Hamjui tarifa hiyo ilimathiri vipi yeye na familia yake pengine ndio kilichopelekea yote mliyaona na kuyasikia leo. Baba aliniambia siku zote tunakosea ili tujifunze, yaani ukiumia utatafuta njia ili usiumie tena, ukilia utatafuta njia ili usilie tena. Kwangu mimi naamini hiki hakitakuja kutokea tena, sio kwasababu nimeshapoteza,hapana kwasababu nakijua.
Eva akaendelea kujibu maswali na mwishoni akazindua toleo jipya la nguo mbili, ambazo moja aliita Father na nyingine Mother. Watu walinunua sana sana na sana, na kuvunja rekodi za mauzo.
***MWISHO***
"SIO KILA SINGLE MAMA CHANZO NI BABA"
Peter Charlz
Comments (1)
See all