Please note that Tapas no longer supports Internet Explorer.
We recommend upgrading to the latest Microsoft Edge, Google Chrome, or Firefox.
Home
Comics
Novels
Community
Mature
More
Help Discord Forums Newsfeed Contact Merch Shop
Publish
Home
Comics
Novels
Community
Mature
More
Help Discord Forums Newsfeed Contact Merch Shop
__anonymous__
__anonymous__
0
  • Publish
  • Ink shop
  • Redeem code
  • Settings
  • Log out

Riba za Shonde

Kuendea Ras

Kuendea Ras

Sep 20, 2021

‘Aah mzinga imeisha!’ Hiyo line ndio ilianzisha stori yote,ikikatiza stori Shonde alikuwa anapeana kuhusu ati siku alibebwa na wasee kwa roadi,akatupwa kwa ndae,akapelekwa kwa keja fulani akadungwa madawa na akarudishwa.Walikuwa kwa keja ya PAULO.Paulo ndio nikama alikuwa bola wa hii mbogi juu alikuwa dere wa mat.Mat yake.Kulikuwa na madem kadhaa lakini walikuwa washazima kwa viti,viti za mat zilikuwa zimejaa kila pahali, ni tu dem mmoja alikuwa amechill  na Paulo wakichoma,wakiskiza Riba za Shonde.Spare parts za ndae zilikuwa kila pahali,Paulo alikuwa anazitumia kama decoration.

Ilikuwa Friday usiku, keja ilikuwa nikama imewashwa moto.Moshi kila pahali hadi hawakuwa wanaonana fiti. ‘Weh shonde mazee kuna maji na kuna pombe, maji ni ya kutoa kiu na pombe ni ya kulewa,sionangi kama wewe unajua hivo.’ MESI alikuwa ameuma ndimu akizulia Shonde juu ya kumaliza mzinga.Walikuwa Shonde, Paulo na Mesi kwa hiyo keja. ‘Weh enda udenki, nitakunywa vile nataka, pombe ni maji na maji ni pombe…Ata ilikuwa kiasi tunafaa kuongeza ingine,’ Shonde alizulia Mesi na kasauti fulani ka kulazimishwa.‘Saa nne ishafika...’ Paulo akadai akiwa na ki king size kwa mkono,uso yake imefichwa na moshi, ‘..mtapatana na GODE huko nje na ata baze zote zishatingwa.’

Wote walinyamaza,kila mtu kwa kiti yake,. ‘Ah zii hatuwezi kuwa rada hadi mona…zii…riba za shonde si za kuskizwa mtu ukiwa rada…,’ Mesi akadai, ‘…Si RAS ako.Si tunaweza enda tumstue atukindie.’ ‘Sa unadai kumuamsha sahi?’ Paulo akamuuliza. ‘Hawezi kuwa amelala sahi,Leo ni Friday, tuende tumchukue kwake, tufike kwa wines  yake,atukindie,hivo tu na turudi…huyu ni Ras,ka kitu imampea dooh hawezi zua,’Mesi akadai. ‘Weh mimi siendi na nyinyi, na siwapei gari mwende kushikwa huko,Gode anajua vile ata hii gari huguruma.’ Paulo akazua. ‘Ah weh Paulo acha hizo,…’ Mesi akamskizia, ‘Kila mtu anajua Gode hakuwangi Friday…ata utakaa huku ukifanya nini na huyo dem wako ashazima.’ Paulo akageuka akacheki dem akizima pole pole akiwa ameshika blunt inatoa moshi kati kati ya vidole.Paulo akaichukua bila kumuamsha, akaizima. ‘Mbona ata mnadai pombe na nimejaza mashada huku,’ Paulo akadai,akipoint bag ya shada yenye ilikuwa kwa meza.Meza ilikuwa imejaa vumbi ya shada kila pahali.Pia kulikuwa na lighter fulani moto, glow in the dark, hapo kwa meza. ‘Ah zii mazee,nadai kuchangamka,Friday ni siku ya pombe.’ Mesi akasema atakaa alijua Paulo alikuwa ashaingia box.

Walitoka nje wakigoja Paulo ageuze mat.Kulikuwa na harufu ya makaa inachomwa kila pahali.Bizna ya kuchoma makaa ni moja ya zile bizna za gizani.Ukiifanya usiku,hiyo moshi humezwa na giza,kitu inabaki pekee ni harufu.Kulikuwa na moon chini ya clouds sa kulikuwa na light kiasi ya kuona kwenye unakanyaga tu.

Shonde alikuwa na mwili ndogo sa alipenda kuvaa majacket kubwa kubwa ndio akae mbigi.Lips zake zilikuwa black,na hakuwa na meno kadhaa.Mesi alikuwa na jezi pekee,akatoka dem mmoja hapo jacket yake.Mesi alikuwa anaitwa Mesi juu vitu mingi.Kwanza,juu alikuwa ameivisha futa,futa ya mdomo.Pili,juu msee angeamua kukucheza,angekucheza,vibaya,lakini si madem,nasema dooh na vitu ka hizo.Mesi ni wale tu masurviver,hakuna ngori hangeweza kujitoa,kwanza ya makarau.Sa hizo vitu mbili zinaonyesha mbona yeye ni Mesi lakini sasa yenye ilifanya aanze kuitwa Mesi in the first place ni juu ya kubet.Mesi alikuwa addicted na kubet.Lakini hakuitwa Mesi juu ameivisha kubet,ni hiyo njia ingine, kila kitu yenye alikuwa anawekelea ilikuwa inaogelea yote,sa wasee,kumbeba ufala,wakaamua kumuita Mesi.Ni siku moja tu yenye kila mtu anajua Mesi aliwahi kula,juu alilewesha mbogi yote hapo Space,klabu ya mtaani.Unacheki,kitu ya ufala ni ati kwa hii mbogi yote ya kina Paulo,Mesi pekee ndio alikuwa na job...job,job ya ukweli.Alikuwa mechanic mnoma,alikuwa hadi amesomea.Lakini juu ya kubet,msee hakuwahi kuwa na dooh,ata mwisho ya mwezi.

Mat ya Paulo ilikuwa zile Mat zenye zinaweza kufikisha kwa mlango  yako,atakaa unaishi ndani ya shimo. Paulo alikuwa dere mnoma,budake pia alikuwa dere wa mat lakini yeye alikuwa ameandikwa kwa sacco.Hii mat ya Paulo haikuwa na karibu kila kitu ma license,nini...By kuwa kwa roadi tu alikuwa anavunja rules ka zote.Kama kuna mtu alichukia makarao kabisa hii Kenya,ni Paulo,juu ya ufala zenye amefanyishwa sana sana na karau mmoja wa mtaa.Karau anaitwa GODE.Jina ya ukweli ya Gode ilikuwa ‘Nduro’.Hiyo area hiyo jina ilikuwa inatetemesha kila mtu.Lakini kwa mayut,alikuwa anaitwa Gode,na ni Paulo alimpea hiyo jina.Paulo husema ati kuna type kadhaa za makarau na ukizijua,utaweza kusurvive kwa roadi.Moja,na ile ya kawaida ni mwenye ukimjenga dooh,ni hivo,hatazua.Pili,ni mtiaji,mwenye actually anafuata rules,najua ni ngumu kuamini wako,lakini wako.Sa ukipatana na huyo,weh pigia tu corner mbali,utumie njia ingine.Hao wawili ukiwajua  uko sawa,kutoka hapo utajua vile utafanya.Sa kuna type ya mwisho,na ni karau tu mmoja ako kwa hiyo type,Gode.Hii ndio ile mbaya kabisaa,yenye huwezi predict nini anataka.Kuna time anadai dooh,kuna time anajifanya mzuri ukitoa dooh anaweza ata kuweka pingu,na kuna time amechizi tu.Aliwahi cheki Paulo akipigia corner mbali badala ya kuwachia akaingia kwa mariamu akaanza kumkimbiza kama kwa movie.Paulo alimchukia hadi akampea hiyo jina,Gode.Paulo hudai ati,Gode, na msee amehepa mathare,akavaa uniform za karau,hakuna difference.

 Paulo pia amevurugana na wasee wa mat mara kadhaa, siku ingine karibu wamchomee gari juu ya kuwaibia macustomer.Watu walipenda kubebwa na Paulo juu hakuwa anatambua unaenda wapi,bora utoe pesa za maana.Unaweza jiuliza nini Paulo alikuwa anafanya na mbogi ya watu kama Shonde na Mesi.Alijuana na Shonde akiwa Mtoi na walikuwa highschool moja na Mesi lakini hakuwa anashinda nao juu ya hiyo.Unacheki Paulo hakuwa na bro ama siz.Maisha yake yote imekuwa tu yeye na wazae wake na hiyo kitu imeishi kumsumbua.Sa Paulo hapendi kukaa pekee yake ata kidogo,ukiweza enda keja yake,wakati wowote utapata kuna mtu huko atakama Paulo mwenyewe hayuko.Anakuwanga pekee yake tu akidenki ama akishower.

Sa walijisunda kwa mat ya Paulo, na wakatokea.Mesi aliketi kando ya Paulo na Shonde akaingia huko nyuma kwa viti za wasee.Akaketi nyuma ya kiti ya dere,ya Paulo.Hakukuwa na kitu imegawanisha side ya dere na ya passangers,sa walikuwa wanachekiana fiti.Hawakuwasha headlights ndio wakuwe chini ya maji.Gari ilienda tu pole pole,ikimezwa na giza hadi ikapotelea ndani.Hiyo area ilikuwa ushago ushago hivi,ni kama nje ya tao.Sa kulikuwa na Mashamba,maploti,mabush na misitu ndogo ndogo.Kulikuwa kumenyamaza,ilikuwa tu masauti za wanayama wa gizani na hiyo sauti ya mat ikiguruma.

‘Cheki Paulo, huingizii hao madem tumewacha huko wanaweza kutoka?’ Mesi akauliza Paulo. ‘Ah zii, hao wako nje ata sidhani wanaweza tembea,na ata nimewafungia huko ndani.’ Paulo akajibu. ‘Ni akina nani ata? Walitoka wapi?’ Mesi akauliza.Paulo akadai ‘Ebu uliza Shonde, yeye ndio alikam nao.’ Mesi akaangalia Shonde,Shonde alikuwa  tu fanto,macho nje ya window,mdomo imefura side moja karibu ilipuke,alikuwa anachana.Mesi akamuuliza, ‘Cheki,Shonde,hao madem ni akina nani?’ ‘Madem…ooh,hao magaldem wako kejani?....hao tuliwaokota mchana,walikuwa nnnjeeeh,nikama walitoka bash iliangukiwa na makarau juu ya corona,sa walikuwa wanasaka baze ya kuendeleza sherehe,hapo sa ndio nikaingia,nikafukuza mandume walikuwa nao,nikaleta madem.’ ‘Alafu ukafanya wazime juu ya kuongea mingi.’ Mesi akamgeuzia. ‘Mesi bado umecatch juu ya pombe…tunaendea ingine usianze kulia.’ Shonde akamrudishia.

‘Unacheki makarau pahali?.....eeh….Paulo..,’ ‘Mmmh’ ‘Unacheki makarau pahali?’ Shonde akauliza Paulo. ‘Weh,mimi ata sioni shet! hakukuwangi na giza mob hivi,hii ni ufala mnanifanyisha lakini mkona bahati juu najua hii roadi vizuri….’ Paulo akasema.

Mat ilikuwa tu inasonga pole pole tu kwa hiyo giza.Ikienda juu na chini ya mawe zenye zilikuwa kwa roadi.Shonde akiangalia nje pia yeye alicheki,hakukuwangi na giza hivo. Hii sio tu giza,kuna kama kimoshi Fulani pia,Shonde akajiambia.Wote walikuwa wamenyamaza,Paulo ako rada ya roadi,Mesi ameketi tu anaangalia mbele kwa giza na Shonde,amewekelea kichwa kwa dirisha akiangalia nje na jaba kwa mdomo.Sa unacheki Shonde,Shonde huamini anakuwanga na kitu fulani,sijui naweza iita aje,nikama kipawa hivi,yenye hajawahi ambia mtu yeyote kuhusu.Ni kama anawezanga kusense hivi,kujua kuna ngori kabla ngori yenyewe ifanyike,ndio maana yeye pekee ndio hubaki kuambiana stori.Sa akiwa tu hapo,akiangalia nje,mat tu ikisonga kwa hiyo giza-moshi,alipata hiyo feeling,hiyo kitu anaskianga kabla kuharibike.Lakini akaona awachie tu,juu kuna time anaskianga hivo na kitu mbaya haifanyiki na pia ata angeambia akina Paulo,haingefanya waache kuenda juu walikuwa washatokea.

Walifika kwa gate ya ploti ya Ras,Paulo alizua kuingia ndani,akashow akina Mesi na Shonde waende wamchukue,yeye awategee nje.Sa juu gate ilikuwa imetingwa,ilibidi wameiruka,wakaenda pole pole hadi keja ya Ras.Kulikuwa kumewaka blue ndani na hapo juu ya mlango,chini ya rooftop juu ilikuwa ploti ya floor moja pekee,kulikuwa na bulb ilikuwa imemulika hiyo area ya mlango pekee.Sa Shonde akiwa tu karibu kungonga ngonga kwa mlango,Mesi akamkatiza,akaenda kwa maskio yake,akamshow ‘Cheki,amewasha light ya blue.’ Shonde akamwangalia akishindwa nini msee anasema.Sa Mesi akaongeza ‘Si ni wewe unasemanga ati mtu ukipata msee amewasha light ya blue kejani either ako mechi ama ananyonga.’ Shonde aliinua kichwa yake akisema ‘Oooh’ bila kutoa sauti alafu wakaenda kwa window,wakainama kuchungulia ndani.Curtain ilikuwa imejikunja kiasi,ikaonyesha corner moja ya kitanda ya Ras.Harufu ya shada na kondole zilikuwa kila pahali kwa hiyo window.Ras hakuwa anaonekana lakini kulikuwa na dem juu ya hiyo bed,walikuwa wanaona tu kutoka tumbo yake kuenda juu,alikuwa na bra pekee.Alikuwa anamove juu na chini pole pole.Akina Shonde hawakuwahi ona kitu kama hiyo tena kwa maisha yao,alikuwa mweusi,skin yake ilikuwa inaglow blue-black under hiyo light ya blue.Urembo.Ilikuwa kama kuangalia malaika mweusi.Akina Shonde walichangwa karibu wasahau nini ilikuwa imewapeleka huko.Kenye iliwarudisha rada ni kuona miguu  za mwanaume chini ya huyo dem.

Sa Mesi na Shonde walikuwa kwa do-a,wakidai sa kuknock.Shonde akainua mkono pole pole kugonga lakini Mesi akashikilia mkono yake, akamwambia kitu kwa maskio,alafu Shonde,mara moja,akarudi kwa window kuchungulia.

Paulo alikuwa kwa gari,amejinyamazia. Kulikuwa tu na masauti za crickets,madogi zinabweka huko mbali na wanyama wa giza.Alitoa ndom ya white akacheki awategee akivuta,akaanza kusaka lighter,lakini nikama haipati.

Sa Mesi,alinua mkono yake pole pole,akiipeleka kwa mlango alafu mara moja akagonga ngonga nanguvu ‘Du!Du!Du!’ akishout ‘Kijana! unavuta bhangi! fungua hii mlango!’Shonde akiwa kwa window alicheki Ras ameruka akatupa dem kando kama amesimama.Macho zake zilikuwa kama tochi za gari,alikuwa ameingizia.Shonde kucheki hiyo uso ya Ras alipasua unyama hadi akadunda chini,akapiga magoti.Makeja hizo zingine ziliwashwa light,nikama waliamsha maneighbour.Ras na yeye kuskia msee akiisha nje,alivaa short mbio kama amefungua mlango na akatoka nje.Alikuwa kimsee kirefu hadi alikuwa ameblock light ya hiyo bulb ilikuwa hapo.Giza ilificha mabega zake kwenda juu lakini kulikuwa na mwangaza ya kutosha ya Mesi na Shonde kuona uso yake kiasi.Alikuwa na macho za white na madredi nono refu.Alifungua hivi mlango kama amecheki Shonde.Uso yake ikaanza kukunjika kunjika,akaanza kukondoa macho.Alikuwa amewaka moto.ALIKUWA AMEJAM.Shonde aliacha kucheka,akiwa tu amepiga magoti,akainua kichwa yake kuangalia Ras.Uso yake,uso ya Shonde,Mesi kwa maisha yake yote hakuwahi ona Shonde akiwa ameingizia hivo,uso yake ilikuwa tu uwoga.Ras alisonga mbele kuendea Shonde.Mesi akaruka mbele yake kumsimamisha,‘Cheki Ras…Ras achia tu…tulia…’Ras kuona Mesi,akasimama,alafu akaangalia Shonde.Akaona zii,akaendelea kuskuma Mesi akidai, ‘Shonde tumezoeana….tumezoeana vibaya….leo sikuwachii msee.Nakutoanisha.’ ‘Cheki ras,chill, Shonde ni fala…Shonde ni fala ata wewe unajua hivo…cheki…cheki...tumekuja biashara.’ Ras kuskia hivo alisimama,akaangalia Mesi alafu akaangalia Shonde.Shonde hakuwa amesonga hadi kidogo. Ras bado hawachii,anaendelea kuskuma Mesi. ‘Cheki Ras tungekuwa tunavuruga Shonde kila time akifanya ufala si tungekuwa tushammada sahi…muachie tu,’ Mesi akaendelea kumskizia.Ras akasimama,akaangalia Mesi.

‘Mnadai nini?’ Ras akauliza. ‘Tunadai mzinga.’ ‘Mmefanya hii ufala yote juu ya mzinga!’Ras akazua. ‘Mazee ni saa nne,tunafaa kufanya nini usiku yote bila pombe.’ Ras alinyamaza,angalia Mesi alafu akatupia macho Shonde.Saa hiyo,kutoka kwa hiyo shimo kwa window, yenye Shonde alikuwa anachungulia,manzi wa Ras alikuwa amekalia bed,mgongo kwa wall,amejifunika na blanketi,kichwa pekee ndio ilikuwa nje.

Ras aliangalia Mesi, alafu akasema ‘Sawa’,akageuka kurudi ndani.Mesi akasmile lakini Ras akasimama mara moja,akaangalia Mesi. ‘Hamnunui mzinga moja, mnanunua tatu….sawa?’ Mesi alinyamaza wakaangaliana na Ras. ‘Sawa’, Mesi akasema na sauti ndogo.Ras akageuka na akarudi ndani.

‘Babe,hao ni akina nani?’ Dem akauliza Ras. ‘Ah ni wasee Fulani tu.’ Ras akajibu akivaa nguo. ‘Cheki usinibebe ufala, tuliamua tutakuwa tunaambiana kila kitu,’Dem akacheki ras anavaa. ‘Kwani unaenda?’ Ras,akiwa amevaa nguo,akaketi kwa bed,kando ya dem akamshika mkono,akamshow,‘Itabidi nimetoka kiasi.’ ‘Sahi?unatoka nje kufanya nini sahi?...leo ilifaa kuwa tu sisi,mimi na wewe’ Dem akadai. ‘Najua,pole…ni bizna..unajua vile kumekuwa…na tunahitaji dooh.’ Ras akamskizia. ‘Basi ata mimi naenda na wewe,’ Dem akadai. ‘Zii, cheki..huko nje ni rada chafu, curfew ishafika na sijui nini inaweza happen nikishatoka huko nje,weh nitegee hapa…ukule,nilipika food na ata hatukukula,ulifika kama tumeanza….’ Wote walismile, karibu wacheke. ‘…cheki tuko pamoja weekend mzima…na nikirudi…’ Ras akamkaribia akamwangalia macho, ‘…nitakufanyia ile kitu unapendanga.’Dem aliblush. ‘Sawa…..enda…lakini ujichunge…urudi kwangu.’ ‘Lazima,’ Ras akasema.

Mesi aliingiza kichwa kwa mlango haraka,akacheki wakimunju alafu akarudisha.Shonde alikuwa anajaribu kuamka kutoka baze alikuwa.Hakuwa anaskia mwili yake kutoka kiuno kwenda chini.Aling’angana kiasi kabla aweze kusongesha mguu,mwishowe,akaweza kusimama.Akarusha mikono zake kwa mifuko haraka.Alijiambia ni njeve, kujiskizia tu, lakini ndani alijua ukweli.Vile aliweza kutembea,akaenda kusimama kando ya Mesi,akamshow,‘Unajua wewe ni nini? Weh ni haga.’

Sa Ras,Mesi na Shonde walikuwa wanatoka karibu wafike kwa gate,wakacheki mzae fulani,mmoja wa maneighbour wa Ras.Alikuwa metoka nje kuzua juu ya makelele.Sa alikuwa hapo nje anawaangalia akidai kuzua lakini vile akina Ras walimtupia macho mzae alisare tu akarudi ndani kwa bibi yake.Ras akafungua gate,na wakatoka.

Kufika kwa gari,walipata haina mtu.Mat ilikuwa tu hapo,milango zimetingwa,Paulo hayuko.Alafu kiasi kiasi wakaskia makele gizani kutoka kwa bush fulani ilikuwa tu hapo mbele ya alafu Paulo akatokea kati kati ya giza-moshi,akitoa moshi kwa mdomo,alikuwa anavuta fegi. 'Weh..rada?' Mesi akamuuliza.


simbamwizi
karuirukariithi

Creator

#Lighter #paulo #mesi #ras #shonde #karuirukariithi

Comments (0)

See all
Add a comment

Recommendation for you

  • Blood Moon

    Recommendation

    Blood Moon

    BL 47.6k likes

  • The Last Story

    Recommendation

    The Last Story

    GL 43 likes

  • Secunda

    Recommendation

    Secunda

    Romance Fantasy 43.3k likes

  • Silence | book 1

    Recommendation

    Silence | book 1

    LGBTQ+ 27.3k likes

  • What Makes a Monster

    Recommendation

    What Makes a Monster

    BL 75.3k likes

  • Invisible Boy

    Recommendation

    Invisible Boy

    LGBTQ+ 11.4k likes

  • feeling lucky

    Feeling lucky

    Random series you may like

Riba za Shonde
Riba za Shonde

1.5k views4 subscribers

A night out past curfew
Subscribe

6 episodes

Kuendea Ras

Kuendea Ras

259 views 4 likes 0 comments


Style
More
Like
List
Comment

Prev
Next

Full
Exit
4
0
Prev
Next