Please note that Tapas no longer supports Internet Explorer.
We recommend upgrading to the latest Microsoft Edge, Google Chrome, or Firefox.
Home
Comics
Novels
Community
Mature
More
Help Discord Forums Newsfeed Contact Merch Shop
Publish
Home
Comics
Novels
Community
Mature
More
Help Discord Forums Newsfeed Contact Merch Shop
__anonymous__
__anonymous__
0
  • Publish
  • Ink shop
  • Redeem code
  • Settings
  • Log out

Riba za Shonde

Wines and Spirits

Wines and Spirits

Sep 28, 2021

Paulo akadai ‘Ah….umh…nilii..nilikuwa kunyora…nyi watu mmekaa, kwani mlienda kupikiwa chai huko ndani?...’ Akaona Ras, ‘Ah… Ras, uko aje?’ Ras akamwangalia tu, nikama bado alikuwa amejam.Shonde aliangalia Paulo, akamwangalia akienda kwa mlango ya driver na akiingia.Kulikuwa na kitu tofauti kumhusu.

Waliingia mat na wakaendelea na mishoni. Ras aliketi huko nyuma, nyuma tu ya kiti ya Mesi na Shonde alikuwa nyuma ya Paulo. Walikuwa wamekaribiana, Ras na Shonde, lakini walijaribu yao yote macho zao  zisipatane. Sa ilikuwa kufika kwa baze ya Ras.Haikuwa mbali na kwenye walikuwa.Shonde sahi alikuwa ashatulia, hakuwa na haja ya kuficha mikono juu zilikuwa zimewacha kutetemeka. Gari ilienda ndani ya giza, ikikata hiyo giza-moshi mara mbili na ikimezwa nayo kutoka nyuma.Walikuwa wamenyamaziana, kila mtu akili yake ilikuwa mbali.Paulo alikuwa anashinda akiangalia lighter fulani nzee ya silver ilikuwa juu ya dashboard.Mkono yake ya left ilikuwa kwa steering wheel, ya right ilikuwa imeshikilia fegi. Mesi alikuwa anashindwa watapata pombe saa ngapi juu zake zilikuwa zishaanza kushuka. Ras alikuwa anafikiria kuhusu manzi wake, kuhusu vile hiyo usiku haikuwa inaenda vile alikuwa amepanga.Shonde na yeye alikuwa anafikiria kuhusu…Shonde alikuwa anafikiria kuhusu nini?

Gari ilikuwa tu inawatingiza ikienda pole pole, juu na chini ya mawe, kila mtu akitingika kivyake. Light ya green ya speedometer na ya red ya buttons zenye zilikuwa zinafanya ndio light pekee ilikuwa ndani ya  hiyo gari.

‘Ras sikujua ukona dem.’  Mesi alikatiza hiyo silence. Ras bado alikuwa anaangalia mbele through windscreen. Alinyamaza tu. ‘Ras ukona dem?’ Paulo aliuliza akigeuka akamwangalia alafu akaangalia mbele. Ras alismile,akasema, ‘Ata mimi sikujua nikona dem, nilijipata tu.’ ‘Waah, yaani Ras akona dem’ Paulo alijisemea akiangalia mbele, akidrive na akivuta fegi, alikuwa ameshukisha window yake tu kiasi ndio moshi itoke nje lakini yote ilikuwa inachapa Shonde huko nyuma. ‘Kwani sifai kuwa na dem nini?’ Ras akawauliza. Paulo akachapa puff bigi, alafu, ‘Ah zii…’ moshi ikitoka kwa mdomo akiongea, ‘…ni vile ukiwa hiyo baze yako ulikuwa unapita nao, mtu hangesema wewe ni mtu wa kuweka dem kejani, uko poa msee, tumefika hizo miaka.’ Jivu ya fegi iliangukia steering wheel na trouser ya Paulo.

Kurudi nyuma kiasi, vile   Mesi na Shonde walikuwa wameendea Ras wakawacha Paulo kwa Mat akiwategea,Paulo bado alikuwa anasaka lighter kwa gari hadi akatoka kuisaka kwa mifuko akijipanguza jivu. Nje kulikuwa tu masauti za crickets,madogi,na yeye kusema ‘Shit’ vile alicheki alisahau kubeba lighter wakitoka kejani.Aliiwacha hapo tu kwa meza. Akiwa karibu kurudi ndani ya mat, ndio akaskia masauti  kutoka kwa bush ilikuwa tu hapo mbele. Alafu kukanyamaza. Ilikuwa nikama sauti za wasee wakibonga, sauti za madem. Alirudi kwa kiti yake ya driver, akafunga mlango, aka breath out. Kukaa kukaa, akaziskia tena, this time akaskia vizuri, ilikuwa sauti ya dem akicheka. Akaamua kuenda kucheki, kuona ka ni wasee wanachoma magizani wamuokolee lighter.

Alikuwa anatembea pole pole kwa edge ya roadi, karibu na hiyo bush. Akafika baze aliskia hizo sauti, hakukuwa na mtu.Huko ndani kulikuwa na miti zimeunda kamsitu fulani hapo tu kando ya ploti ya kina Ras. Kiasi tu, akaona nguo ya white, ikipeperuka kiasi kwa mti.Nikama kulikuwa na mtu amesimama hapo, lakini hiyo side ingine ya mti.Hiyo nguo, haikuwa tu white pekee,Paulo aliona nikama ilikuwa inaglow kwa giza, kama bulb. Paulo alijipata akiingia ndani,akienda hapo.Alitembea akifuata hiyo nguo juu hiyo ndio kitu pekee alikuwa anaona vizuri kwa hiyo giza-moshi. Alikwaruzwa na miti akijaribu kuifikia. Hakunotice, lakini alikuwa anaenda ndani na ndani ya  msitu.

Alisimama mara moja, kuenda kuangalia nyuma,akaskia sauti za dem akicheka tena,akaangalia mbele mara moja,akaona mtu amesimama kati kati ya rows mbili za miti.Sijui ka ni juu ya giza lakini hakuwa anaona uso yake vizuri.Na sio uso pekee,pia mikono na miguu, ilikuwa tu figure ya black imeform shape ya kichwa na mwili ndani ya hiyo dress.Kitu pekee alikuwa anaona ni macho zake. Zilikuwa circles mbili bigi za white na dot ya black ndani.Dress yake ilikuwa inamulika kila kitu hapo ikipeperushwa na upepo kiasi.Ilikuwa kubwa,imeflow hadi kwa ground. Paulo alianza kutembea haraka, karibu kukimbia, akimwendea, akategwa na mzizi ya mti akaangauka akiangalia tu huyo dem.Nikama ground ilikuwa inajisongesha.Alisimama haraka, akamwangalia tu. Alijipata akiwa amepotea ndani ya macho zake. Bila kujua alijipata amevutwa hadi mbele ya huyo manzi akiangalia tu macho ,ama manzi alijipeleka hadi mbele yake,hangejua gani ni gani.Kuna kitu kuhusu huyo manzi yenye ilikuwa familiar.Alikuwa anaskia kama ni mtu ashawahi patana na yeye pahali kitambo,lakini hakumbuki lini na wapi.Macho zake zilikuwa nikama zinavuta Paulo ndani yake.Alikuwa anaskia kitu ashawahi skia kitambo,alikuwa amekaa sana bila kuskia hivo,hakuwa anataka kutoka hapo.Ilikuwa the same feeling alikuwa anapata mzae wake akirudi home weekendi akitoka job.Hiyo harufu ya fegi na nyama choma.Mzae wake hangewahi kosa kubeba nyama choma, kunyeshe ama kuende aje. Hapo,dakika tu kiasi,alikuwa ameskia kama amerudi kwa nyumba ya wazae wake akiwa mtoi.

Paulo alikuwa amepotea kwa macho za huyo dem,alafu,mara moja,akaskia makelele za mlango ikigongwa kwa ploti ya kina Ras,akageuka kuangalia hiyo side.Kurudisha macho zake kwa dem,akapata hayuko.Alikuwa amedisappear,kitu ilikuwa imebaki ni hiyo nguo ya white,imejikunja kutengeneza circle  na ndani ya circle kulikuwa na kitu inashine,inareflect hiyo light ya dress.Kuangalia,akapata ni lighter,akaichukua, alafu akaangalia mbele.Alikuwa tu pekee yake.Aliangalia hiyo lighter,akaiangalia na akaikumbuka. Aliwahi kuwa na lighter kama hiyo kabisaa.Ya silver,imekwaruzwa kwaruzwa.Ilikuwa kwa vitu za mzae wake zenye waliletewa vile mzae wake alikufa kwa accident.Zilikuwa hiyo lighter na cassettes kadhaa za rhumba.Mzae wake hangewahi endesha gari kama rhumba haichuni kwa radio.Lakini Paulo alitokwa hiyo lighter akiwa kwa chain fulani,huko tu mtaani. Alikumbuka vile hiyo story ilikuwa imemuuma. Hakuwahi achia hao wasee, hadi wangemuitia bag mzima hangewahi enda. Alijaribu kuiwasha na ikawaka, akaingia kwa mfuko yake akapata ile ndom ya white.Akaenda kuiwasha,akawacha. Akarudi kwa mfuko, akatoa packo ya mafegi, alikuwa anavuta fegi kama zenye tu mzae wake alikuwa anavuta, akachukua moja na akaiwasha. Aligeuka kuangalia nyuma, akaona ata hakuwa ameingia ndani sana. Akajipanguza vumbi na akaanza kurudi.Vile alitokea kwa roadi, alipatana na akina Ras nje ya gari.

Waliendelea safari wakiwa wamenyamaza.Githaa, hapo chini ya shimo yenye radio ya mat ilifaa kuwa, ilikuwa inasema 11:30 lakini Ras bado alitoa kabambe yake kuangalia ilikuwa saa ngapi. Ilikuwa imebaki kiasi wafike hiyo baze ya Ras. Mesi alikuwa amenyamaza akaiangalia tu mbele.Alikuwa anaswing miguu zake left-right.Mkono yake ya right ikiwa juu ya mguu yake ya right.Alikuwa anasugua magoti yake  pole pole, chini ya dashboard. ‘Kwani hatufiki,’ Mesi akasema akiwa tu ameangalia mbele.Ras alikuwa anapiga mao kwa akili, wafike, awamalizie haraka haraka, isipite dakika tano alafu arudi teke kwa mrembo wake.Ras alikuwa amejizoesha kupanga vitu kwa akili kutoka kitambo sana. Unacheki Ras, yeye ni mmoja ya wale watu kiasi  hii dunia wenye wanaweza sema wamejijenga kutoka zero.Ras alielewa umuhimu wa dooh akiwa tu mtoi.Wazae wake walimpata wao wenyewe wakiwa watoi.Sa dooh imekuwa shida maisha yake yote.Hakujua vile wazae wake waliweza ata kumpeleka chuo.Akiwa class six, aliwahi kaa chini,akapiga hiyo mao,akacheki atahitaji kulipiwa ryma hadi iishe,alafu highschool miaka nne,alafu tena campo. Hiyo kitu ilikuwa inamsumbua.Siku moja akiwa class seven, alihepa chuo akarudi home mapema.Vile alifika home,alijua vile masake alikuwa akipata hizo dooh za chuo.Alichukua bag yake,akaweka vitu zake  na akahepa home na hakuwahi rudi tena.Akaenda hiyo mtaa ya kina Paulo.

Miezi za kwanza,alidoz nje na machokoch.Hapo ndio akajua kusurvive.Hizo siku alikuwa tu mrefu,hakuwa na madredi lakini hakuna mtu anakumbuka jina yake kabla aanze kuitwa Ras.Unacheki,yeye hakuwahi keti chini akaamua ati kuweka dredi.Hakupenda kunyoa nywele tu.Hakuna kazi hii dunia Ras hajafanya.Kuna time akiwa mjei, na jioni,akitoka job,alikuwa anafanyia pedi kazi.As in,alikuwa anaokolea pedi kukinda ngwai zake,anapewa commission kulingana na vile ameuza.Lakini zilikuwa manyaru sa hazikuwa zinaenda sana.Kuna time ingine alikuwa anapika kwa hoteli.Hizi hoteli za mtaani zenye hauhitaji kuwa umesomea bora chakula yako inakulika.Sa hapo urefu yake ndio ilimuokolea,hakuwa anakaa miaka zake.Alifanya hapo miaka  kadhaa.Alipenda hiyo job,kupika,ilikuwa inamsaidia kufikiria.Kama ingekuwa na dooh za maana,angeifanya maisha yake yote.Hiyo time pia alikuwa ameweka kuku kejani,alikuwa anazipea food yenye ilikuwa inawachwa kwa hoteli.Lakini sa hiyo ilibacko juu hizo kuku zilikuwa fupi,kuku ya miezi tatu ilikuwa inakaa kuku ya mwezi moja na zilikuwa zinataga mayai kama ya nyonde,ndogo.Hiyo time hakujua,lakini ilikuwa juu ya kukosa jua.Mwishowe,na dooh zenye alikuwa amemake kwa hoteli,akaamua kuingia bishara ya ngwai,vizuri sasa.Vile alikuwa anafanyia pedi kazi,alicheki vile hiyo bizna ikona dooh,na hiyo time ata ilikuwa manyaru,akajiuliza, Na basi shada ya maana? Alitaka sa kuifanya vizuri, kujipandia na kujiuzia.Akaanza na kufanya research kwa mneti,akasoma kila kitu kuhusu science ya shada.Akasaka mbegu,mchanga fiti,akanunua lights,fans na akatengeneza kabaze kadogo ndani ya keja yake.Ilikuwa keja bigi.Ilikuwa kazi mingi lakini shida moja kubwa yenye alikuwa nayo ni makarau.Alijua hiyo lazima ingemsumbua,lakini, alikuwa anakinda baze different kila time ndio asijulikane baze moja haraka.Hapo ndio alijuana na kina Paulo,hiyo time,Paulo ndio alikuwa customer wake mkubwa kabisa.Hizo siku, Paulo angeshika ngwai ya kapa kila wiki.Hii ni kabla ajue kushika bag na Ras hangejaribu kumchanua.

Kila mtu mwenye alikuwa anachoma hizo siku alikuwa anajua Ras.Ras pekee ndio alikuwa na shada ya maana hiyo area.Vile Ras aliendelea kujulikana, ndivo aliendela kumake dooh mingi na pia ndio aliendelea kujipata kwa ngori.Sio tu makarau,hadi mapedi wengine walikuwa wanadai Ras akuwe pedi wao.Ras alikaa akacheki,hiyo ni cartel alikuwa anaanzisha,na hiyo haikuwahi kuwa kwa mao zake.Alikuwa anadai kusare,kuingia bizna rada safi na hapo ndio akapatana na msee anaitwa ALVO. Unacheki vile Alvo alimaliza diploma yake, mzae wake alimjenga  20k na akamwambia hataki kuwahi ona uso yake karibu na yeye tena.Sa alikuwa anasaka baze ya kutumia hizo dooh kabla azichome zote kwa pombe na madem.Paulo akamconnect na Ras.Wakaamua kuanzisha hiyo wines and spirits na dooh zenye walikuwa nazo.

Walifika.Wines and spirits ilikuwa room moja pekee,imejengwa pekee yake,ikona milango mbili,moja mbele,ingine nyuma.Hiyo area ni mbali na tao sa hakukuwa na makeja mingi.Zenye zilikuwa hapo zilikuwa zimewachana wachana.Nyasi ilikuwa imemea kwa hizo spaces sa wasee walikuwa wameunda paths za kuconnect hizo makeja.Kulikuwa kunakaa fiti,kama ungeenda hapo mchana.Kutoka mbele ilikuwa inakaa area rada safi.Lakini kutoka nyuma,kila wall ilikuwa imechorwa graffiti na dem fulani kichwa mbaya alikuwa anaitwa Achieng’ lakini wasee walikuwa wanamuita ARCH. Arch alikuwa amenyoa kabisa.Alikuwa na nose-ring na ma tatt kila pahali kwa mwili yake.Yeye na mbogi yake hawangewahi achia wall safi.Ilikuwa inawawasha kuona tu wall safi.

Lakini kwa wall ya wines, Ras mwenyewe ndio aliita Arch akamshow achore hapo kenye anadai. Kwa wall ya mlango ya nyuma.Alimshow angemlipa, Bora ikuwe kitu inapiga kelele, hivo ndio Ras alisema exactly.Arch kuskia hivo, alichangamka vibaya.Walienda mafichoni,wakachoma hadi zikashika ile kabisa,wakarudi. Wakaseti bluetooth speaker hapo, wakachunisha magenge oldschool,wakaikalia. Arch alichora simba bigi imejaa kwa wall yote, ikiwa imefungua mdomo, inadishi mtu mwenye nitu miguu zake zimebaki zikihang nje.lakini badala ya kuweka nywele za kawaida,akaichora ikiwa na madredi zimehang hadi kwa walls za sides.Hiyo kitu ilibamba Ras mbaya. Lakini tena, kuna vile Arch alichora huyo mtu anadishiwa, vile ukifungua hizo milango za nyuma, ilikuwa inakaa nikama anapanua na unaingia kati kati ya miguu zake.

Hapo kando kulikuwa na hoteli fulani bigi.Wasee walikuwa wanajichocha wanaenda huko sherehe wanapata hawawezani na  hizo bei, wanajipata wamejisunda baze ya Ras wakichapa makali.Sa Ras aliunda ka kibanda huko nyuma akaweka viti na meza za plastic,vitu portable,juu hiyo area haikuwa yake,ilikuwa ya kanjo,sa kanjo wangewahi tokea,hiyo baze ilikuwa inadisappear nikama haikuwahi kuwa hapo.

Paulo alificha gari huko nyuma, kati kati ya kibanda na hiyo wines, alafu wakatokea. Mesi, Shonde na Ras wakaenda kwa mlango. Paulo alitoka kwa gari akakaa hapo nje, akilalia mlango ya kiti ya Mesi akicheki akina Ras wakienda kufungua mlango.Alitoa ile lighter kwa mfuko.Akaiangalia,alafu akaanza kucheza nayo,anaiwasha anaizima,anaiwasha,anaizima,akiangalia hiyo moto. Ras alitoa key na aka kufungua lock.Mara moja tu akaskia makelele huko ndani ya vitu zikianguka na zikisongeshwa.Makelele hazifai kuwa baze imetingwa.Akavuta mlango haraka na akaingia.Kulikuwa na giza,kumenyaza Ki! Akatupa mkono kufikia switch na akawasha light.Ikawaka green,akaona, MACHO.

 

simbamwizi
karuirukariithi

Creator

#Lighter #Made_in_Kenya #kenya #wines_and_spirits #ras

Comments (0)

See all
Add a comment

Recommendation for you

  • Blood Moon

    Recommendation

    Blood Moon

    BL 47.6k likes

  • The Last Story

    Recommendation

    The Last Story

    GL 43 likes

  • Secunda

    Recommendation

    Secunda

    Romance Fantasy 43.3k likes

  • Silence | book 1

    Recommendation

    Silence | book 1

    LGBTQ+ 27.3k likes

  • What Makes a Monster

    Recommendation

    What Makes a Monster

    BL 75.3k likes

  • Invisible Boy

    Recommendation

    Invisible Boy

    LGBTQ+ 11.4k likes

  • feeling lucky

    Feeling lucky

    Random series you may like

Riba za Shonde
Riba za Shonde

1.5k views4 subscribers

A night out past curfew
Subscribe

6 episodes

Wines and Spirits

Wines and Spirits

223 views 1 like 0 comments


Style
More
Like
List
Comment

Prev
Next

Full
Exit
1
0
Prev
Next