Kulikuwa na macho kila pahali.Macho zimekondolewa zinamulika Ras kama headlights za magari,parts za white za macho zikireflect green ya bulb. ‘Ah ni Ras, hee….’ Msee akatokea akijaribu kubreath na kuongea at the same time ‘…hee msee….hee karibu nigenye.’ Ilikuwa Alvo,alikuwa amewekelea mkono yake ya right juu ya moyo yake.Kiasi kiasi watu wakaanza kujitoa mafichoni.Ilikuwa mbogi.Kumbe wasee walikuwa sherehe huko ndani.Ilikuwa akina Arch,mabeshte wengine wa kina Ras na mlevi yoyote mwingine wa hiyo area.Wines and spirirts iliwatapika wote nje,wakajaa hapo.
‘Alvo nini mbaya na wewe? Unakumbuka vile tulitoboka last time Gode alitupata huku ndani…alafu unakunywa kwa job…nini shida yako?’ Ras akazulia Alvo. ‘Ah weh ni Friday, Gode hakuwangi leo, si ata wewe ulikuwa fom zako….alafu cheki, hawa watu wote…’ Alvo akageuka akipoint na mkono yake, ‘…mazee singeachia,tunahitaji kucheza hizi mishoni ndio tusurvive.’ Alvo akajitetea.Ras akamwangalia, alafu akageuka kuangalia wall.
Juu walikuwa side ya nyuma, chupa za mizinga zilikuwa kila pahali kwa wall. ‘Mesi ako?’ Ras akauliza akiangalia angalia
‘Eya!’ Mesi alijibu, alikuwa ashaketi kwa table ilikuwa hapo na tambler kwa mkono. ‘Kujia vitu zenu,’ Ras akamshow akiwa ameshikilia mzinga kwa mkono moja.Alafu mara moja,akairudisha kwa wall na hapo ndio Mesi alinotice,kwa wall,kwenye chupa zilikuwa zinawekwa,haikuwa kabati ama kitu kama hiyo. Zilikuwa michongo za mbao uso za watu wanapiga nduru,midomo ziko wazi na wamekondoa macho nikama wameona kitu hawaamini mbele yao.Zilikuwa nyeusi zote,uso za mbao nyeusi kwa ukuta zinakaa kama watu mwili zao zilimezwa na ukuta. Sa mesi alicheki Ras akirudisha pombe kwa wall,akacheki akiingiza chupa unyama ndani ya mdomo ya hizo uso. Mesi aliiangalia,alafu akaangalia Ras,ilikuwa inakaa kama hizo uso zinamwangalia zote juu yeye ni mrefu na alikuwa hapo ndani,nikama yeye ndio amezistua hivo.Mesi kucheki hivo, alijipata ametoka nje mara moja,akiwa analimp kiasi,akasimama kwa mlango akaangalia angalia,nikama anasaka msee.Hiyo light ya green ilikuwa imemulika nje kiasi.Akacheki Shonde,hapo tu kando ya mlango, alishaingia kwa chain na akina Arch, mbogi ilikuwa huko ndani.Alafu akacheki Paulo,amesimama kwa mat,akiwa amelalia mlango kiasi,akiangalia lighter,akiiwasha na akiizima.Mesi akaenda hadi kwake. ‘Cheki Paulo, unaitwa na Ras.’ Paulo akaweka lighter kwa mfuko, akaenda, akawacha Mesi hapo kwa gari.
‘Kwani ni mimi nalipia hizi mizinga? Mesi ako?’ Paulo alizua na akatoka nje kusaka Mesi.Hakumwona pahali.Akaangalia Shonde akipeana stori, akamwangalia, akakatizwa na Ras. ‘Weh Paulo! Teketisha,sina usiku mzima hapa’ ilibidi Paulo amelipia,akijiambia atadai Mesi hizo dooh lakini ndani alijua hiyo ni giza tu. ‘Si tuvuke’ Paulo akaambia Ras. ‘Sirudi na nyinyi sahi, siwezi achia walevi hii place.Nyi endeni, nitajirudisha nikishafukuza hawa watu.’ Ras akadai.Paulo akatoka nje na mizinga kwa bag. ‘Weh Shonde! Tuende! Na Mesi ako?’ ‘Sijamcheki,’ Shonde akajibu. Lakini alikuwa amemcheki, walikuwa wameangaliana Mesi akipita Mat akienda kwa kibanda.Mesi alipita hapo mbio,na tambler imejaa pombe kwa mkono.Aliskia Arch akizulia Shonde juu ya kuongea hadi anasahau ni yeye akona shada kwa mkono,inabidi wameshinda wakiiwasha.
Paulo alitupa hizo mizinga kwa hiyo kiti ya Mesi.Akaingia ndani, na akaanza kugeuza gari.Shonde aliingia na wakakaa hapo wakitegea Mesi.Paulo akaanza kusongesha gari. ‘Weh kwani tunaacha Mesi.’ Shonde akazua. Paulo aliendelea tu kuvukisha Mat, bila kutambua.Shonde akashout nje ya window, akiambia Mesi anawachwa.Wakiwa tu karibu kutoka hiyo baze,Mesi akatokea kutoka kwa giza akiwakimbilia kutoka nyuma.Paulo akasimamisha gari,Mesi akaingia na wakavuka.
‘Msee ulikuwa denki nini? Karibu Paulo akuwache,’Shonde akashow Mesi. Mesi akaangalia Paulo.Paulo alikuwa tu amenyamaza,akiangalia mbele.
Mesi,kabla arudi, alikuwa amekalia kiti kwa kibanda,amestretch mguu yake ya right,anasugua magoti akifunga macho nikama anaskia uchungu.Alikuwa gizani lakini light kiasi ya green ilikuwa inafika hapo.Akisugua tu mguu,aliangalia juu yake mara moja na akaona kitu imehang kutoka kwa mbao zilikuwa zimeshikilia karatasi huko juu.Akaangalia vizuri akacheki ni bat.Bat ilikuwa imehang upside down,imejikunja hapo.Aliiangalia akaona macho zake ndogo zikishine green-black,zikimwangalia pia, lakini alikuwa amewahi skia pahali ati bat zinakuwanga vipofu, sa, hakuogopa.Alijisahau akiiangalia alafu mara moja akakatizwa na sauti ya Shonde ikimuita,ikimwambia atawachwa,akachapa pombe yote yenye ilikuwa kwa tambler mara moja na akatokea.
‘Weh Mesi, najua kenye umefanya…,’ Paulo akageuza kichwa kiasi kutoka kwa bara bara,akaangalia Mesi, ‘…mizinga tatu ata ni za nini na unajua mi huwa sikunywi’ Mesi aliziangalia,alikuwa amezitoa kwa kiti akaziweka chini. ‘Weh hukunywi lakini madem wako si hukunywa.Utawapea zenye zitabaki badala ya kushika zingine.’ Mesi akamshow. Paulo akarudisha kichwa kwa barabara.
Paulo alikuwa amemaliza miaka mbili bila mdomo yake kupatana na pombe.Aliwacha tu mara moja na hajawahi onja tena.Yeye hupeleka mat yake ifanyiwe service kila mwezi ndio iweze kuingia shimo zenye yeye huiingiza.Sa asubuhi moja,mat ikiwa service kwa garage yenye Mesi alikuwa job,yeye na Mesi,wakitegea imaliziwe na hao fundi wengine,walienda kutoa lock baze ya Mathe.Shonde na yeye alikuwa ameenda kupigania jaba huko nyuma ya tao kwa stage,jaba ilikuwa tu imefikishwa saa hiyo.Ilikuwa inategewa na vijana wote wa mtaa.Sa Paulo,akacheki badala ya kukaa pekee yake,avuke na Mesi baze ya Mathe kuchapa chemison.Kwa hiyo mtaa,hiyo hiyo ndio ilikuwa chang’aa fiti kabisa.Akina Paulo walikuwa wanakumbuka mathe ako siku zenye walikuwa wanadai zishike na wamesota.Hizo siku walikuwa wanapiga sherehe vibaya,karibu kila siku.Lakini hiyo asubuhi ata hawakukunywa sana,wateja wa Paulo walishinda wakimpigia simu ikabidi aingie job,akawacha Mesi hapo kwa garage.
Sa Paulo alikuwa kwa barabara za huko ndani,mbali na tao,amevuka kuvuka ndio asichelewe kuendea wateja wake,mara moja tu,akacheki mtoi juu ya windscreen yake.Hakuwa anaamini,alikuwa amegonga mtoi.Ata hakuwa amemwona kwa roadi yenyewe,alimcheki tu juu ya windscreen. Alimgonga, akamvunja miguu.Kama angechelewa kumfikisha hosi,angededi.Kutoka hiyo siku,Paulo hakuweza kudrive kama mwezi mzima,alikuwa anaingia kwa gari anaguza steering wheel anaanza tu kutetemeka.Ata angejilazimisha kuendesha,alikuwa anafika tu kwa barabara hivi,moyo yake inaanza kupiga haraka na anashindwa kusongesha miguu,anashindwa kunyanga mafuta ama brake.Inaweza kosa kuwa juu ya pombe,pengine atakama angekuwa rada bado angegonga huyo mtoi lakini bado alijichukia juu ya hiyo stori,akaamua kusare tei kabisa. Lakini mwishowe ilibidi ameendesha juu lazima hustle iendelee. Pole pole akaenda akizoea.Lakini bado hadi sahi,akiamka tu asubuhi aingie kwa gari,kitu ya kwanza kwa akili yake huwa ni hiyo siku,hajawahi sahau.Sasa yeye ni mtu mashada na fegi pekee.
Walikuwa kwa safari ya kurudi keja ya Paulo.Ilikuwa imebaki dakika kadhaa ifike saa siata usiku.Giza ilikuwa imeongezeka, giza ama moshi, hungejua.Harafu ya kuchoma makaa bado ilikuwa kila pahali,mbwa pia hazikuwa zimetulia ata kidogo.Zilikuwa zinabweka, zingine zinatoa masauti akina Shonde hawakuwa wamewahi skia tena. ‘Weh mimi sioni kitu,itabidi tumewasha mataa.’ Paulo akadai. ‘Washa! Kama kuna masanse tungekuwa tushawacheki,’ Mesi akamshow. Shonde alikuwa ameketi kwa window, amejinyamazia. Alidai kusema kitu lakini nikama aka sare.Paulo akawasha mataa.Zilimulika area kidogo ya barabara,hapo tu mbele yao. Haikuwa imewekwa lami.Imejaa mawe na vumbi na sides zote mbili kulikuwa na fence ya kei-apple.Waliongeza speed kiasi,wakaanza kutingishwa tingishwa.Mawindow zikaanza kupiga kelele.Shonde alikuwa anaskia njeve,alikuwa amejikunja kwa kiti.Bado hakuwa anaskia fiti.Alijaribu yake yote kutoa hiyo feeling lakini haikuwa inatoka.Kuna kitu mbaya ilikuwa karibu kufanyika.Mesi alikuwa amefungua mzinga,anaikunywa kutoka kwa chupa.Walinyamaziana na kelele za mbwa na wanyama wa gizani, ‘Hizo dogi zinakulana nini?’ Mesi akasema alafu akageuka kuangalia nyuma,akaangalia Shonde.Alafu akamwaga pombe kiasi kwa tambler akampatilishia. ‘Cheki Shonde,mbona mbwa zihulia hivo usiku?’ akauliza Shonde.Shonde aliangalia tambler,ikiwa bado kwa mkono ya Mesi,alafu akaangalia Mesi.Akaichukua. ‘Huwa inasemekana ati dogi zihuweza kucheki vizuri usiku,kuliko watu. Na sa vile ni usiku,kumenyamaza,pia huwa zinaskia vizuri.Naskianga ati zinalianga hivyo juu ya kuingizia,juu huwa zinaweza kuona na kuskia vitu za usiku….’ Shonde akasema. ‘Vitu za usiku?’ Mesi akauliza akiwa tu amegeuka. ‘Unacheki usiku,kuna vitu huwa zinatoka mafichoni,vitu zenye sio za hii dunia na dogi huwa zinaweza kuziona na kuziskia,sa huwa zinalia juu ya kuogopa,zikijaribu kutuchanua lakini sisi sa hatuelewi lugha ya mbwa.’ Shonde akamshow. Mesi alinyamaza tu akimwangalia,alafu mara moja,Paulo akaisha, ‘Shonde unadai Mesi ashindwe kulala.’ Paulo alisema alafu akaangalia ile lighter ya chuma,ikiwa hapo juu ya dashboard.
Mesi akiwa tu amegeuka,akiangalia nyuma,nyuma ya gari kupitia hiyo window ya nyuma.Akacheki kitu huko nyuma yao. Kulikuwa na giza sa hakuwa anaona fiti lakini ilikuwa inakaa kama gari.Akajaribu kuangalia vizuri.Akacheki ni gari,lakini haikuwa tu gari ya kawaida,haikuwa imewasha mataa na… ‘Oya oya oya oya Paulo Paulo Paulo Paulo..,’ Mesi akasema,akigonga gonga bega ya Paulo,bado akiwa ameangalia nyuma, ‘..KUNA MARIAMU NYUMA YETU.’ ‘Acha ufala!Walai?’ Paulo akasema akijaribu kuangalia nyuma. Shonde alikuwa ashageuka akiwa amepiga magoti kwa kiti.Vile tu aliiona, alijua,hakuwa amekosea,hii ndio imekuwa ikifanya askie vibaya kutoka usiku ianze. ‘Shet!...sahi ndio hawa mafala wanatokea!…Tukirudi!’ Paulo alisema akiongeza speed. ‘Mazee aki isikuwe Gode,aki Mungu walai isikuwe Gode…’ Paulo akasema akiwa rada ya roadi mbaya, mikono zote mbili kwa steering ‘…na nilijua tu,hakuna vile huyo fala angewachia….lazima tu angetokea leo…siku yenye pia mi niko nje…lazima tu! Siniliwaambia? ’ Paulo alikuwa nikama amechizi,anajibongesha akikanyaga mafuta kukanyaga.
Mesi alikuwa bado hapo kati kati ya kiti yake na ya Paulo.Shonde alirudi kwa kiti yake.Tambler bado kwa mkono, hajaikunywa. Tei ilikuwa imemwagikia kiasi juu ya ile mbio Paulo alikuwa anaenda.Walichomoka mbio, nyuma walikuwa wafuatwa na vumbi lakini hawangeiona.Walikuwa wameenda hadi hawakuwa wanaona kitu yoyote nyuma yao.
Shonde hakuwa anaskia fiti.Mesi na Paulo walikuwa wanabambika tu vile wameacha hiyo mariamu nyuma lakini kulikuwa na kitu inaambia Shonde wasianze kusherehekea.Alikuwa anaskia njeve hadi na jacket alikuwa amevaa.Mara moja tu, Shonde akasema, ‘Paulo simamisha gari.’ Mesi akamwangalia. ‘Ati!’ Paulo akaamuuliza.Shonde akabreath out, ‘Najua…najua…lakini….weka gari kando ya roadi,na uzime mataa.’ Paulo, bado akiwa amekanyaga mafuta na akiangalia mbele ‘Umefiat msee! mwishowe jaba zako zimekuweza, umekula majani hadi ukakuwa mbuzi…hiyo mariamu ikitufikia,hii usiku yote imeharibika…zii ata..ata …ata si leo pekee, weekendi yote,zii.. hii mwezi yote ata juu tutatoboka tusote mwezi mzima.’ Paulo akadai namavurugu, akijaribu kuwa rada ya barabara na akijaribu kuambia Shonde. ‘Cheki najua…najua lakini mazee….cheki…sijui nitawaambia aje,lakini niaminieni hapa mazee,mara tu hii moja muwache kuniona ka fala,’ Shonde akajaribu kuwaskizia.Mesi akaangalia Shonde,akamwangalia githaa kiasi alafu akaangalia Paulo akasema, ‘Tusimame Paulo.’ ‘Ah zii…zii…hakuna vile nasimama…nyi mko zenu…unajua tukishikwa hakuna kitu nyinyi mtapoteza,’ Paulo akadai, kichwa yake bado ikiwa tu kwa barabara. ‘Ata mimi kesho asubuhi lazima nikuwe job,nikikosa nitamalizwa..’ Mesi alisema, akiwa tu hapo, akiangalia Paulo alafu akageuka akarudi kuangalia nyuma, ‘…cheki ata hawa wasee wakiweza amua kutufuata hadi kejani wanaweza, hakuna mtu mwingine kwa barabara na wako tu hapa nyuma yetu,wacha tufanye vile Shonde anadai...,’ akaangaliana na Shonde ‘….kukienda vibaya,ni yeye atatoboka.’ Mesi akamalizia. Paulo alibreath out,akaangalia kwa kioo ya hapo juu,akacheki huko nyuma ni giza tu,alafu,bado kwa kioo, akaangalia Shonde,Shonde alikuwa anaangalia nje kwa dirisha,Paulo akamwangalia alafu akaslow down.Shonde akanotice gari inaslow down akaangalia mbele kwa kioo,macho zake zikapatana na za Paulo. ‘Sawa…nitasimama, wacha tuone vile kutaenda, kama ni Gode,mjue tushajitomba,Mesi ficha hizo mizinga,wakizicheki hawataziachia,’ Paulo akasema bado akiangaliana na Shonde. Shonde alikuwa tu anaona macho zake, hangejua kama alikuwa ameuma ndimu ama ka alikuwa tu kawaida, lakini macho zake zilikuwa zinaogopesha.Mesi akatupa mizinga huko chini kabisa,mwisho ya miguu.Ilikuwa kando kabisa ya roadi sa mat ilikuwa imeinama side moja,side ya Mesi.
Comments (1)
See all