Walikuwa wamezima gari na mataa, sa walikuwa ndani ya giza. ‘Alafu nini Shonde?’ Mesi akauliza akiwa amepinduka kuangalia Shonde. Na sauti ndogo,Shonde akasema, ‘Mnyamaze,kabisa,mtu asisonge,msikohoe…mnyamaze kabisa.’ ‘Kwa nini?...’ Paulo aliuliza na ukali, ‘Mbona tufanye hizo vitu unatuambia,mbona ata tunakuskiza?’ Shonde alinyamaza kwanza,alafu ‘Juu kuna kitu nimekumbuka,story fulani….lakini nitawashow baadae,sahi tu nyamazeni na mniaminie.’
Wote walikaa kwa viti zao na wakanyamaza.Ilikuwa tu wao,mat,giza na zile vitu za giza. Mesi aligeuka pole pole akaangalia nyuma na akaicheki,alafu akarudi.Hakuwa amekosea,ilikuwa imewafuata hapo tu nyuma yao. Walikuwa wamenyamaza ki! Hungesema kulikuwa na watu hapo ndani. Mariamu ilikuwa inasonga tu pole pole,ikipanda mawe za barabara na ikishuka.Haikuwa imewashwa mataa.Ilifika tu hapo nyuma yao,imebakisha kama tu metre moja iwafikie.Shonde aliaanza kutetemeka mikono.Hakuwa anaskia kitu kutoka waist yake kuenda chini.Alikuwa nikama amepigiliwa misumari kwa hiyo kiti,hangeweza kusongesha hadi kidole.Moyo yake ilikuwa inapiga hadi akaanza kuskia harufu ya damu kwa mdomo yake.Mariamu sa ilikuwa ishawafikia huko nyuma,inapita kando yao pole pole tu.Hapo ndio Shonde alijua, kulingana na vile alikuwa anaskia,alijua,hii ngori walikuwa sahio,haikuwa ya kawaida na akajiambia kimoyomoyo, Huyu sio Gode, zii, NI KITU MBAYA ATA KULIKO GODE.
Ikiwa tu kando yao, kabla haijafikia Paulo, ndio Shonde, kwa corner ya macho yake, aliiona. MARIAMU YA WHITE. Sa hiyo tu,ripples zikaanza kutokea kwa pombe alikuwa nayo kwa mkono.Kulikuwa na moshi ya white kila pahali, hadi ndani ya mat. Hiyo mariamu, haikuwa white pekee, Nikama tu yule dem wa msitu. Paulo alisema kimoyomoyo vile ilifika kwa dirisha yake. Ilikuwa inaglow white kila pahali kama bulb. Mikono za Paulo zilikuwa kati kati ya miguu, chini ya steering, zinatingika. Alikuwa anaskia vile tu aliskia akiwa na yule dem kwa msitu, nikama anakumbuka kitu. Kukumbuka feeling.Alikuwa anaskia vile aliskia ile siku aligonga yule mtoi. Kujichukia na kuregret. Alijaribu kukunja vidole zake pamoja lakini hazikuwa zinawacha kutetemeka. Shonde sasa alikuwa ashajua kabisa,hii ndio ile kitu mbaya yenye ilikuwa ihappen.Alikuwa amesema wasimame lakini vile hiyo mariamu ilikuwa hapo, alianza kujishuku,pengine hawangesimama.
Mara ya mwisho yenye Shonde aliskia vile alikuwa naskia saa hiyo, ilikuwa akiwa mtoi,akiwa ryma. Siku moja,akiwa tu chuo, alipata feeling tu mbaya,hadi akashindwa kucheza na classmates wake. Jioni vile alikuwa anarudi home,kuenda tu kufungua mlango ya gate ya ploti,mkono ilikuwa nikama inakataa kusonga.Vile alifungua na akaingia,alipata kumejaa watu nje na ndani ya nyumba.Mzae wake alikuwa hapo nje ameketi pekee yake.Aliangalia tu Shonde,akamwangalia, alafu angaalia kwingine. Masa ya Shonde alikuwa amejinyonga.Aliishi kuwa mgonjwa sa walikuwa na bill kubwa hospitali hawakuwa wamelipa.Aliacha barua akisema sa,Shonde na budake hawatateseka tena juu yake.Hiyo ndio mara ya kwanza Shonde alifikiria kuhusu kifo lakini kutoka hiyo siku,ata hiyo siku yenyewe,Shonde na mzae wake hawakuwahi ongea kuhusu masake tena.Hawakuwahi ongea ata kuhusu kitu yoyote tena.Kila mtu alikuwa maisha yake.Hiyo ndio mara ya mwisho aliskia vile alikuwa anaskia hiyo mariamu ikiwa hapo, kando yake.
Ikiwa tu karibu kupita Paulo, mguu ya Mesi ilikuwa imeanza kutingika.Alikuwa amegonganisha meno zake za juu na za chini pamoja,amefunga macho.Magoti yake ilikuwa imewaka moto.UCHUNGU.Mariamu ilikuwa inapita pole pole,karibu ipite Paulo,mguu yake ikajisongesha,ikaguza mizinga huko chini ‘CLING!’ Mariamu ikasimama.Ilikuwa hapo tu kando ya Paulo.Dirisha yake,kwa dirisha ya mariamu.Mesi aling’ang’ana, akageuza shingo tu kiasi,kuangalia,akitetemeka na aking'ang'ana kupumua pole pole.Dirisha za mariamu zilikuwa black ndani,hungejua kama ni tint ama nitu giza. Mesi alianza kukumbuka vile alipata shida ya magoti,vile aliskia hiyo siku. Alikuwa form four, walikuwa holiday, mzae wake alikuwa ameenda safari akawacha truck yake home.Ilikuwa ndogo, ya kubeba vitu za shamba.Mzae wake hakuwa arudi hadi wiki iishe.Buda ya Mesi alikuwa mtiaji,ile utiaji hadi alikuwa anafungia Mesi ndani ya nyumba na padlock.Hawakuwahi skizana juu ya stori ya Mesi kushinda na mamechanic time ya holiday.Mzae wake alidai asome,akuwe sijui doki, hizo vitu kila mtu husema. Sa vile alivuka, Mesi alicheki akona wiki ya kufanya vile anataka na hakuna kitu ingine ilikuwa kwa akili yake. Akaita Paulo,wakafungua engine ya lori.Hawakuwa na haraka juu walikuwa na wiki mzima. Siku moja tu kabla wiki haijaisha, mzae wake alitokea tu hapo,mbele yao,parts za lori ziko kila pahali chini .Hakuzua ata,aliingia ndani ya hao na akaketi.Lakini vile Paulo alirudi kwao, mzae wake aliendea fimbo walikuwa nayo,ati ya kuvuruga wezi.Hiyo usiku, Mesi alilala akilia.Alikuwa amepigwa ka dogi.Mwili yake mzima ilikuwa inauma lakini ni place moja alipatwa vibaya kabisa na hadi sahi haijawahi acha kuuma,magoti yake.Hakuwahi ambia mtu yeyote kuhusu hiyo stori,hadi Paulo.Lakini hivyo ndio Mesi alidhani.Ukweli ni aliwahi ambia Shonde siku fulani wakiwa wamelewa na Shonde hajawahi sahau.
Wote walikuwa wanapitia siku zile mbaya kabisa kwa maisha zao na sio tu kukumbuka,kuskia vile waliskia hiyo siku.Lakini kulikuwa na kitu ingine ilikuwa inaendelea.Vile hiyo mariamu ilikuwa hapo,kando yao,walikuwa wanaskia nikama inawavuta. Kila muscle kwa mwili yao ilidai tu kufungua mlango na kutoka.Shonde alikuwa anaomba mmoja wao asilemewe,mtu asitoke.Mariamu ilikaa hapo dakika kama mbili alafu ikaendelea.Lakini hizo dakika mbili zilikuwa kama siku mzima. Pole pole, ikizungukwa na hiyo moshi ya white,ikiglow ndani ya giza,ikaenda ikimezwa na usiku.Ikawacha akina Paulo vile tu walikuwa.Wamenyamziana,kila mtu kwa akili yake.Walikaa hivyo kama dakika tano bila kusonga ama kuongea. Alafu Paulo akatoa mikono yake chini ya dashboard.Akaziwekelea kwa steering.Bado zilikuwa zinatingika kiasi.Alishikilia steering nanguvu alafu akagurumisha gari na wakatokea.Hakuna mtu alijaribu kuongea hiyo njia yote.Kila mtu alikuwa ametulia.Paulo alikuwa anaendesha pole pole,gizani bila kuwasha mataa.Hangejaribu kuziwasha.Mesi pekee ndio alikuwa anafanya kitu,alikuwa anameza pombe kama maji.Kukunywa ilikuwa inamsaidia na uchungu.Alinotice hakuwa anaskia uchungu sana zikiwa zimeshika.Shonde alikuwa tu amenyamaza,alafu ndio akacheki amekuwa na pombe kwa mkono hiyo githaa yote.Akaichapa.
Walifika kejani na Paulo akapark gari.Walikaa ndani ya gari kwa parking,wamenyamaziana.Kila mtu alikuwa bado anajaribu kuelewa kenye kimefanyika. Mesi alitoka, akiwa amebeba mizinga.Alitembea akistagger karibu adunde.Wote walienda hadi kwa mlango,na Paulo akafungua.
Vile waliingia ndani,walipata kumechangamka. Kulikuwa kumewashwa stima na hakukuwa na moshi mingi vile waliacha kukiwa. Marooti zilikuwa zinachuna kwa system,ilikuwa radio ya mat.Kulikuwa na madem kila pahali.Wawili kwa meza,choo ikaflash, mwigine akatokea. Wengine bado wamezima kwa three-seater ya mat yenye ilikuwa hapo chini ya dirisha.Kwa dirisha kulikuwa na maua zimepadwa kwa container za mbao.Lakini maua moja ndogo kwa vase ya orange,haikuwa maua,ilikuwa shada. Sahi,bila moshi ndio ungecheki hiyo keja vizuri.Ilikuwa keja bigi.Marim za gari zilikuwa zimehangiwa around walls zote. Viti zilikuwa zimechapa,zigine zikona mashimo,zimeraruka,zimechafuka.Meza ndio ilikuwa katikati,imezungukwa na hizo viti zote. Hiyo keja ilikuwanga tu na harufu moja permanent.Mchanganyiko ya harufu ya ngwai na fegi.Kulikuwa na ma ash tray kila pahali, zote zimejaa jivu na filter za fegi.
Akina Mesi walikuwa tu wamesimama kwa mlango,wakiangalia ndani.Alafu Mesi akasonga ndani.Akaenda kwa meza kuwekelea pombe. ‘Ah nyi wasee,kwani mlikuwa wapi?’ Mmoja wa madem wenye walikuwa kwa meza aliuliza vile aliwacheki. ‘Ah,tulikuwa…tulikuwa tu maziara kiasi…..tumeleta pombe,’ Mesi alijibu akiwekelea mizinga kwa meza. ‘Aaah nyinyi sasa ndio mmejua…’ dem alisema akifikia mzinga na tambler kwa mkono,alafu akiweka, ‘..ebu by the way kujeni mtuokolee hapa hivi,’ akapoint meza kwenye ameketi.Walikuwa wanajaribu kuroll ma blunt.Vumbi ya shada ilikuwa kila pahali kwa hiyo meza. Lakini zilikuwa zinawatoka sa walikuwa wanawatch hapo tutorial ya kuroll lakini ata haikuwa inawasaidia.
Haijawahi skia fiti hivyo kuwa ndani ya nyumba,wote,hiyo ndio ilikuwa kwa akili zao.Paulo alienda kwa room yake,akakalia bed,akaangalia hiyo lighter,akaiangalia alafu akaiweka kwa box ndogo ya chuma,hapo ndani kulikuwa na cassettes na mapicha,akairudisha chini ya bed,alafu akarudi kwa kina Mesi.Shonde alikuwa ameketi kati kati ya wale madem wawili,anawashow kuroll. Yeye na Mesi walikuwa wanateremsha pombe wakidai kusahau kenye walikuwa tu wamepitia.Mesi alikuwa tu anaangalia Shonde akikunywa.
‘Cheki, Shonde….’ Mesi akaanza, ‘..kuna riba fulani ushawahi tuambia,kitambo,nimekumbuka tu sahi,riba kuhusu mariamu ya white.’ Kila mtu akaangalia Shonde. Shonde akaangalia Mesi alafu wote wakaangaliana na Paulo. ‘Oh eeh,nilipewa hiyo riba nikiwa mjei,na unajua vile riba za wasee wa mjei zihukuwa,’ Shonde akasema. ‘Ebu tuambie hiyo riba tena,nadai kuskia,’ Mesi akasema.Waliangaliana na Shonde alafu Shonde akasonga ndani ya kiti. Kila mtu alikuwa anamwangalia.
Shonde akaitisha pombe, akachapa, alafu, ‘Sawa basi, kama ni riba mnadai,basi ni riba mtapewa.Lakini hii sio riba ya kawaida,hii sio tu zile stori zenye watu huambiana wakichoma.Zii,hii ni riba nikama zile za kitambo,zile za dunia ya kitambo, zenye mababu walikuwa wanakalisha watoi kwa moto na wanaambia.Sio kuwabamba,zii,kuwachanua,kuwaambia siri za dunia zenye hazikuwa zinaandikwa pahali.’
‘Ilikuwa usiku,usiku kama tu hii ya leo,kulikuwa na giza nzito, nikama moshi ya tire ilikuwa imeshikana hadi ikafanya kukuwe usiku.Kulikuwa na wazae wawili kwa roadi,walikuwa wamelewa mbaya,wanastagger wakirudi kwa mabibi zao, pole pole tu.Hii ilikuwa tu usiku ya kawaida kwao,kutoka kibarua,kulipwa,kupitia Space-kuchapa chupa kadhaa na kurudi kwao usiku pamoja. Nyumba zao zilikuwa zimekaribiana lakini keja ya mmoja wao ilikuwa mbele ya keja ya huyo mwingine.Yaani,mmoja alikuwa anafika mbele ya huyo mwigine.Unacheki mkiwa mmelewa mkiwa wawili ama watu kadhaa,kuanza kufanya hesabu ya sijui nani atalipia nini…ni ngumu mkiwa walevi.Na inaudhi. Sa kenye walikuwa wanafanya,kila mtu alikuwa na siku yake ya kununua,leo ni huyu mzae,kesho ni huyo mwingine.Lakini sasa,mmoja alikuwa amelipia hizo siku mbili za mwisho kufuatana.Na ni huyu mzae mwenye keja yake ni ya kwanza.Sa hiyo usiku,kama kawaida,mzae wa kwanza aliingia kwake na huyo mwingine akaendela kiasi.Lakini huyo mzae wa kwanza vile alifika kwa gate yake,alikumbuka, ah,’ Shonde akainua kidole moja, ‘nafaa kuambia huyo mzae mwingine,yeye ndio analipia ya kesho na ya kesho kutwa juu bibi anazua vile natumia dooh.Akaamua kurudi kwa barabara haraka kumwambia kabla hajaenda sana.Vile alifika kwa roadi,alipata huyo mzae mwingine akiingia gari fulani ya white..,’ Shonde akapeleka kichwa chini kiasi, akaangalia kila mtu,akachapa shot ingine. ‘Sa akajaribu kumuita kabla hajaingia kwa hiyo gari,lakini wapi,nikama msee hakumskia,akaingia ndani na gari ikaenda,alafu skia..’ Shonde akanyamaza, akainua mkono yake akaikunja ngumi ‘…ikadisappear..Pooof!’ Afungua mkono mara moja kama bomb, ‘hivo tu, kwa hewa….The next day mzae anafika Space kulewa na beshte wake lakini msee hatokei.Akachapa machupa kadhaa,lakini sio mingi juu hakuwa na mlevi mwenzake.Akatoka, akafika kwa bibi ya beshte wake kumsaka,lakini bibi akasema ati ata alidhani wako na yeye.Kumbe beshte wake hajaonekana kutoka jana usiku,ndio sa huyu mzae wetu akirudi kwake,akipitia hiyo njia,akakumbuka.Jana usiku,aliona beshte wake akiingia kwa gari ya white.Lakini sahi alikuwa anaiona vizuri kwa akili yake.Haikuwa tu gari,ilikuwa mariamu,Mariamu ya white.Ndio huyo mzae mbio hadi police station kutoa beshte wake.’ Shonde akanyamaza.Akawaangalia tu. ‘Alafu? Kuliendaje?’ Dem mmoja akauliza na wengine wakanyamaza, wakaangalia Shonde nikama huyo dem ameuliza swali ilikuwa kwa akili zao wote. ‘Alafu…ebu nipeeni pombe kwanza,’Shonde akasema.Mzinga ilipitishwa mbio mbio hadi kwa mikono zake.Akainua chupa, akameza pombe dakika kadhaa.Alafu akaishukisha, akaishikilia kwa mkono,akaangalia kila mtu.
Saa hiyo hiyo,Shonde akipeana Riba kwa keja ya Paulo,kitu saa sita na nusu,Ras alikuwa anatoka kufikisha Alvo kwake juu msee alikuwa nje mbaya.Kwa akili yake kulikuwa tu na kitu moja,manzi wake.Sa alitembea pole pole tu kwa giza hadi kwake.Akafika kwa gate na akatoa kifunguo.Akifungua gate,mara moja tu,akawacha.Akasimama straight kama amepigwa radi alafu akageuka akatembea pole pole,bila ata kuangalia,akaenda nyuma ya gari na akaingia.Gari ikaenda,bila kuguruma,bila sauti.Mariamu ya white,ikamezwa na giza.
Manzi wa Ras alikaa kwa meza akimtegea.Alikuwa anajaribu kukula food yenye Ras alikuwa amepika lakini hakuwa anaweza juu ilikuwa karibu saa saba usiku na Ras hakuwa amerudi na hakuwa anachukua simu.
‘Ah siumalizie!’ Dem alikuwa ameshikilia shada bigi kwa mkono alisema,moshi ikitoka kwa mdomo akiongea.Shonde alisonga ndani ya kiti,akajaa ndani,akaangalia juu kwa ceiling.Zilikuwa zimeshika! Alafu akashukisha kichwa,akaangalia huyo dem wa kishada. Akina Paulo walikuwa tu zao, wametulia lakini pia wao wanaskiza. ‘Nilikuwa wapi?’ ‘Mzae ameenda police station,’ dem mmoja,hakuwa ameongea ata mara moja the whole night,akajibu. 'Oooh,…Sa mzae wetu si amefika kwa station kutoa beshte wake.Vile alifika na akashow hao makarao ,walimshow,' Shonde akabadilisha accent, ' Ah! Kuna mzee amezima huko ndani kwa cell siku mzima ata tulikuwa tunashindwa tutamfanyia nini.Mzae wetu si akabambika mbaya,na mzae huyo mwingine akaendewa.Lakini vile tu mzae wetu alimcheki hivi,alisema tu zii,si huyu.Haikuwa yeye.Huyu alikuwa tu mlevi mwingine lakini sio yule beshte wake.Alijaribu kuambia makarau aliona akichukuliwa na mariamu lakini yeye pekee ndio alikuwa hapo na vile makarau waliskia wazae wote wawili,mwenye alihepa na mwenye aliona akibebwa na mariamu ya white ni walevi,waliachia hapo,wakasema huyo mzae ako sherehe na atarudi pesa zikiisha.Lakini mzae wetu hakusare,hakuna vile angesare,yeye alijua kenye aliona.Atakama alikuwa mlevi,alijua kenye aliona.Alianza kukesha hapo,kwenye beshte wake alibebwa.Kila usiku,akijaribu kuona kama Mariamu ya white ingerudi.Siku za kwanza,alikuwa anatoka job,anakaa hapo usiku mzima.Lakini vile githaa ilienda,mzae alianza kuchizi,aliwacha hadi job,akaanza kukaa hapo hadi mchana,akigojea mariamu ya white. Watu walikuwa washazoea,kila asubuhi,wakienda kazi,mzae ako hapo,wakirudi,mzae ako hapo.Lakini siku moja,watu waliamka na wakamkosa….Hivo tu.Mzae hakuwa Space,hakuwa job,hakuwa kwa bibi yake,alikuwa amedisappear.Pia yeye alichukuliwa na kenye ilichukuwa beshte wake. Mariamu ya white.Inasemekana ukiingia Mariamu ya white...
Comments (0)
See all