....wewe ni hivyo.Si ati mwili yako itaokotwa pahali ama kitu ka hiyo,zii, hutawahi onekana tena pahali kwa hii dunia.’
Wote walinyamaza, wakarudi ndani ya viti zao wakiangalia Shonde. Paulo na Mesi pekee ndio hawakuwa wanamwangalia.Sauti ilibaki pekee ni marooti zenye zilikuwa zinaplay kwa background.
‘Aiii…hiyo stori haipelekani’ Dem mmoja, mmoja wa wenye walikuwa wamezima, alisema,nikama stori ilikuwa imemwamsha, ‘sa wanaenda wapi?Hao watu wanachukuliwa,wanaenda wapi?’ Huyo dem aliuliza na kila mtu akaangalia Shonde kugoja jibu. Shonde alisonga mbele kiasi, akawaangalia. ‘Kuna njia moja pekee ya kujua jibu ya hiyo swali, kuingia Mariamu yenyewe.’ ‘Aaah hakuna! Hiyo stori ni chocha tupu,ati mariamu ya white inaenda ikichukua watu usiku….’ Huyo dem akazua akicheka . Paulo, Mesi na Shonde waliangaliana. ‘Naelewa kenye unasema,na ni ukweli,hakuna njia ya kujua kama ni ufala ama ni re-al, juu hakuna mtu ameenda na hiyo mariamu na akarudi.Lakini naweza kuambia hivyo pia.Naweza kukuuliza hiyo swali pia wewe mwenye huamini.Mbona unazua, na pia wewe haukuwa hapo?’ Kila mtu alinyamaza, macho zote zikiangalia Shonde.Shonde alisonga ndani ya kiti,pia yeye akiwaangalia,alafu akasema, ‘Vitu za usiku,ni giza pekee inajua kuzihusu.’
Hiyo usiku, kwa akili za kina Paulo, ilipotea kama giza vile jua ilitokea hiyo asubuhi.Kama tu siku zingine kubwa kwa maisha ya hawa watu, hakuna kitu ilibadilisha.Bado Shonde, Paulo na Mesi watatokea usiku mara zingine mingi.
Wewe kuamini ama kutoamini,haimatter hapa juu hii ni moja ya hizo Riba mob za Shonde.
Comments (1)
See all